DC DEO NDEJEMBI AWATIA NDANI VIONGOZI WA CHAMA CHA CARGO POTTERS WA SOKO LA KIMATAIFA LA MAZAO KIBAIGWA KWA UFISADI.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi Siku 14 zilizopita alitembelea Soko la Mazao la Kimataifa lililopo Mji Mdogo wa Kibaigwa Wilayani Kongwa, katika ziara hiyo aliagiza kusimamishwa shughuli zote za madalali katika soko hilo baada ya Kubaini Madalali huwanyonya Wakulima wanapokwenda Sokoni hapo kuuza Mazao.
Agizo hilo lilipaswa liwe limetekelezwa ndani ya siku 14 na Ndipo DC akajerea na kuwaita Viongozi ili Kujadili.
Baada ya Hapo DC Aliombwa Kikao na Viongozi hao na ndipo DC kaita BODI ya Soko la Kibaigwa, Uwongozi wa CARGO Potters, Meneja wa Soko Kuu la Kimataifa la Kibaigwa, Lengo Kuu nikujadili hali ya Soko na Wafanyabiashara wa Sokoni hapo na Zaidi hao Madalali ambao kwa Kiwango Kikubwa Wamekuwa wakijikusanyia Mapato kinyume cha Sheria na Taratibu.
Wakati kikao kinaendelea kwa majadiliano ndipo DC alipobaini UFISADI Mkubwa ndani ya soko hilo na uwovu unaofanywa na Viongozi hao ndani ya Soko.
DC Alijilidhisha kwa kikao nakubaini haina haja ya kuendelea na Majadiliano bali Viongozi wa CARGO Potters kwa Kuwa Wamekuwa WAKIFISADI ikiwemo kukusanya Mapato kinyume cha Sheria na taratibu tulizojiwekea.Lakini pia wanakusanya Mapato ambayo hayana maelezo yamatumizi yake.
Lakini Pia Viongozi hawa Wamezuia Wafanyabiashara kufanya Biashara zao jambo ambalo Mh DC limemchukiza sana kwani Limefanya Wakulima Washindwe kuuza Mazao yao kwa Amani.Kulingana na Ufisadi huo DC aliamuru kukamatwa kwa Viongozi hao na kumuagiza OCD Kufuata Taratibu za Kisheria ili Wahojiwe na hatua za Kisheria zichukuliwe kulingana na makosa yao hayo yakifisadi.
DC Kawaeleza Wanakongwa kuwa, Yuko kongwa kwa ajili ya kuijenga Kongwa na kuhakikisha Haki na kila namna ya Uwazi inafanyika pasipokuwa na Upindishaji wa Haki zozote, Sheria, Kanuni na Haki zitafuatwa ili Kutenda Haki kwa Kila Jambo. Lakini Kama Ni Majipu Yatatumbuliwa bila Uwoga kwa Maslai ya Kongwa na Taifa kwa Ujumla.
No comments:
Post a Comment