WANAODAI BUNGE KUONYESHWA LIVE WATAKIWA KUOMBA KWA UTULIVU
Katibu
Mkuu wa National Reconstruction Alliance (NRA) Hassan Kisabya Almas
amewataka Watanzania wanaoomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kuonyeshwa kupitia matangazo ya moja kwa moja (Live) kuomba kwa
utaratibu bila kuharibu amani ya Tanzania.
Aidha Katibu Mkuu wa Chama hicho, amesema kwamba amani iliyoko ni hazina kubwa ambayo nchi nyingine inatamani kuwa nayo.
Almas
aliyasema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).
“Leo
hii tupo tunaopigania kutaka kuona Bunge Live, lakini yote haya ni kwa
kuwa Tanzania amani tunayo, sidhani kama nchi kama Afghastan siku
watakayoamua kuonyesha Bunge Live kwa mwaka mzima, kwa saa 24 kama
wataweza kukaa kuangalia Bunge hilo, hivyo basi wale wanaotaka hayo,
kwanza tudumishe amani yetu,” alisema Almas.
Almas
alieleza kuwa, amani ya Tanzania ni zaidi ya dhahabu ambayo Tanzania
inajivunia hivyo ni lazima Watanzania kuitunza na kuithamini amani
ambayo ipo kwa sasa na kuacha kuchochea mambo ambayo yanaweza kuleta
machafuko katika nchi na amani ambayo leo haithaminiwi ikaja kukumbukwa
siku moja.
Pia,
alisema yeye ni mmojawapo wa watu wanaopenda kuona Bunge Live lakini
jambo hilo halishadadii kama inavyofanywa na watu wengine kwani anajua
kwa kufanya hivyo anaweza kuhatarisha Amani ya Tanzania na hata hilo
Bunge halitaweza kuliona tena kutokana na kutokuwa na Amani ndani ya
nchi.
Vilevile,
amewataka waandishi wa habari kuandika yale yaliyo mazuri ya nchi
kuliko mabaya machache ili kuzidi kuitangaza Tanzania vyema kimataifa,
kwani sio uzalendo kuona mambo yote mabaya yanakuwa ukurasa wa kwanza,
bali kwanza yarekebishwe kwakuwa ni makosa yanayoweza kurekebishwa.
Kalamu za waandishi wa habari ni chachu ya amani na maendeleo ya Taifa
la Tanzania.
No comments:
Post a Comment