Wahandisi Temesa wapigwa msasa
kaimu Mtendaji Mkuu Temesa Mhandisi Manase Ole Kujan (wa pili
kushoto) akipata maelezo juu ya ufungaji wa moja ya mtambo wa umeme wa nishati
ya jua (Solar) kutoka kwa Mhandisi Zuhura Semboji mara baada ya ufunguzi wa
mafunzo ya wiki mbili kwa wahandisi na mafundi wa Temesa.
Kaimu Mtendaji Mkuu Temesa
Mhandisi Manase Ole Kujan (katikati) akiangalia moja ya kifaa cha kupimia umeme
kinachotumika katika mafunzo kwa wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa
leo.
Mhandisi Amani Mwanga akitoa maelekezo ya namna ya
kufunga moja ya mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo
ya wahandisi na mafundi wa Temesa
yaliyofunguliwa leo.
Fundi Sanifu kutoka Temesa Mganza Juma (Katikati)akiwa
makini kufunga moja ya mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo
ya wahandisi na mafundi wa Temesa
yaliyofunguliwa leo.
Baadhi ya wahandisi kutoka Temesa wakiwa katika
harakati za kuchuna na kuunga nyaja katika moja ya mitambo ya umeme wa nishati
ya jua (Solar) Katika mafunzo ya
wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.(Picha Zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO).
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO.
Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
wanaendesha mafunzo ya wiki mbili kwa Wahandisi na mafundi wa Temesa ili
kuwajengea uwezo katika kutumia teknolojia ya umeme wa nishati ya jua.
Akifungua
mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mtendaji Mkuu TEMESA
Mhandisi Manase Ole Kujan amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea
uwezo wahandisi na mafundi ili kuweza kutumia teknolojia ya umeme wa
nishati ya jua ambao umekuwa na tija kubwa hasa kwa sehemu ambazo umeme
wa kawaida haujafika.
“Nishati
ya umeme wa jua imeshika kasi kwa sasa na inatumiwa sana katika maeneo
ambayo umeme wa kawaida haujafika hivyo basi kwa mafunzo haya wahandisi
na mafundi wetu wataweza kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuandaa
na kutekeleza miradi itakayosaidia kuondokana na tatizo la umeme
nchini.” Alisema Mhandisi Manase.
Akizungumza
mara baada ya ufunguzi wa mafunzo,Mratibu wa mafunzo hayo kutoka Chuo
Kikuu Dar es Salaam Prof Cathbert Kimambo amesema kwa kushirikiana na
Temesa wameamua kutoa mafunzo kwa wataalamu hao juu ya teknolojia ya
nishati ya umeme wa jua ili kuwasaidia kuendana na mabadiliko ya
teknolojia kwa kuwa na utalaamu na uwezo wa kufanya kazi kulingana na
mabadiliko yaliyopo.
Mmoja wa
wahandisi Kutoka Temesa Bi Sara Moses ametoa wito kwa Wahandisi wengine
kuwa na utaratibu wa kujifunza na kuongeza utaalamu ili kuwezesha
kuendana na mabadiliko Sayansi na Teknolojia katika kuleta ufanisi
katika kazi zao.
No comments:
Post a Comment