MAAFISA WA JWTZ WAMALIZA MAFUNZO KENYA.
Balozi Haule (Katikati) akimpongeza Mwambata wa Kijeshi Ubalozini Nairobi, Luteni Kanali Fabian Machemba. Kulia ni Kanali Msola.
Balozi Haule akizungumza kwenye hafla ya kuhitimisha ziara ya Maafisa wa JWTZ.
Maafisa
na wanafunzi 29 kutoka Chuo cha Kamandi na Unadhimu cha Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Duluti, Arusha, wamemaliza ziara ya mafunzo
ya wiki moja nchini Kenya mwishoni mwa juma lililopita, iliyoandaliwa
kwa ushirikiano na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF).
Kundi
hilo lililoongozwa na Naibu Kamanda na Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha JWTZ,
Kanali Celestine Msola, lilitembelea taasisi mbalimbali za serikali na
Jeshi la Kenya pamoja na taasisi binafsi. Mafunzo yao yalihusu masuala
ya Jamii na Uchumi, Utawala bora, Mfumo wa Kisiasa, Ulinzi na Usalama,
na Maendeleo ya Teknolojia ya Kivita.
Akizungumza
katika hafla fupi mwishoni mwa ziara hiyo, Balozi wa Tanzania nchini
Kenya, Mhe. John Haule, alimshukuru Mkuu wa Jeshi la Kenya, Jenerali
Samson Mwathethe, na watendaji wake, kwa ukarimu waliowafanyia Maafisa
wa JWTZ.
Aliwapongeza
Maafisa hao kwa nidhamu ya hali ya juu waliyoonyesha muda wote, akisema
wameacha sifa nzuri ya JWTZ na Tanzania kwa ujumla.
Mwakilishi
wa KDF, ambaye pia ni Kamanda wa Chuo cha Teknolojia cha Ulinzi, Kanali
Oscar Muleyi, alisema Maafisa wa Jeshi la Kenya wameshafanya ziara ya
mafunzo nchini Tanzania na walikarimiwa vizuri sana.
No comments:
Post a Comment