VIJANA WA KITANZANIA WASHIRIKI MAFUNZO YA UWEZESHAJI KWA VIJANA JIJINI BEJA, NCHINI URENO
Vijana watano kutoka Tanzania ni miongoni mwa vijana 30
wanaoshiriki katika mafunzo ya wawezeshaji wa ujasiliamali unaozingatia
mazingira yanayofanyika jijini Beja, nchini Ureno.
Mafunzo hao ambayo yanafanyika kwa muda wa siku saba
yanalenga kuwajengea uwezo vijana hao kuendesha mafunzo kwa vijana wenzao
katika nchi wanakotoka ili kusaidia kupunguza tatizo la ajira na uharibifu wa
mazingira.
Nchi zinazoshiriki mafunzo hayo na majina ya taasisi
zinazoshiriki kwenye mabano ni pamoja na wenyeji Ureno (Check In), Italia
(Cesie), Argentina (Subiral Sur), Slovenia (Pina), Nepal (CNN) na Tanzania (TYCEN)
ambapo kila nchini imewakilishwa na vijana watano chini ya mradi wa ujasiliamali
wa kujali mazingira ‘Green Entrepreneurship’.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea
kiwanda cha kuchakata taka cha Resialentejo, wakiongozwa na Injinia wa kiwanda
hicho Pedro Sobral.
Wahsiriki wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea
Halimashauri ya Manispaa ya Jiji la Beja ambao walipokelewa na Sonia Calvario
Mshauri wa Meya wa Manispaa hiyo
Mkurugenzi wa TYCEN, Chris Ndalo kutoka Tanzania akitoa mada
wakati mafunzo hayo
Mmoja wa wawezeshaji katika mafunzo hayo, Olga Kuczynska
No comments:
Post a Comment