TAASISI YA MANJANO FOUNDATION WAHITIMISHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MKOANI DODODMA
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Africa na Mkurugenzi wa Taasisi ya
Manjano Foundation Mama Shekha Nasser akieleza Matumizi Sahihi ya
Vipodozi vya Luv Touch Manjano Kwenye Semina ya Ujasiriamali kwa
Wanawake wa Mkoa wa Dodoma.
Awamu
ya Saba na ya mwisho katika budget ya Taasisi ya Manjano Foundation ya
Mafunzo ya Ujarisiamali kwa wanawake 150 kutoka mikoa Mitano Tanzania
yamemalizika Mkoani Dodoma. Wanawake 30 wa mkoa wa Dodoma ni miongoni
mwa wanawake hao 150 walionufaika na mafunzo ya ujasiriamali na namna ya
kupamba kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano.
Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya Biashara wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Manjano. Mafunzo hayo yalilenga kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo na vipodozi. Mafunzo hayo yamefanyika kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza, Arusha na kuhitimisha na Mkoa wa Dodoma.

Pamoja
na mafunzo, kila mshiriki anaunganishwa na mwanamke mmoja mwenye
mafanikio katika biashara au uongozi katika jamii kwa lengo la
kumuongoza katika safari yake ya biashara kwa muda wa mwaka mzima. Baada
ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation
inatoa mikopo bila riba kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha Biashara
wakiwa chini ya Uangalizi Maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la
kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza
kujitegemea.
Wanawake
wa mji wa Dodoma walionufaiki na mafunzo ya ujasiriamali na urembo
wamemshukuru afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na mkurugenzi wa
Taasisi ya Manjano Foundation kwa moyo wa kujitolea na kuwajali wanawake
wengine hususani wakazi wa Dodoma na mikoa ya jirani.
Washiriki walionufaika kwenye Mafunzo hayo wakiwa katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Africa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser.
Wakiongea
zaidi wanawake hao ambao wamepatiwa elimu ya biashara kutambua nafasi
yao katika jamii inayowazunguka pamoja na namba ya kupamba maharusi na
matumizi ya vipodozi.
Wamemshukuru mama Shekha Nasser kwa moyo wenye kuwajali na kuwabeba wanawake wenzake na kutoa elimu ya bure aliyokuwa nayo kwa wengine ili waweze nao kujiongezea kipato na kupunguza ukali wa maisha. Wamemshukuru na wameahidi kuyatumia mafunzo hayo kwa lengo la kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanawake na pia kujiongezea kipato.

No comments:
Post a Comment