Rais Dkt.Magufuli ashiriki kuaga mwili wa Christina Lissu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. Marehemu Christina Lissu Mughwai, alifikwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita, kutokana na Maradhi ya Kansa yaliyokuwa yakimsumbua.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisaini
kitabu cha Maombolezo ya Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye
alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina
Lissu Mughwai, Mh. Tundu Lissu, akisoma wasifu wa Marehemu, wakati wa
shughuli ya kuaga mwili wake, leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar
es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli,
akimfariji Mtoto wa Christina Lissu Mughwai, mara baada ya kutoa taarifa
ya Mama yake.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Aprili, 2016
ameungana na Ndugu, Jamaa na Marafiki kuuaga mwili wa Mbunge Mstaafu wa Mkoa wa
Singida Marehemu Christina Lissu Mughwai
katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.
Christina Lissu
Mughwai aliyekuwa Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Singida katika kipindi cha
kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, alifariki dunia tarehe 07 Aprili, 2016 katika
hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es salaam, alikokuwa akipatiwa Matibabu.
Pamoja na Rais
Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Viongozi wengine waliohudhuria shughuli
ya kuaga mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai ni Naibu Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bunge Mheshimiwa Freeman Mbowe.
Akitoa salamu kwa
niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mheshimiwa George Simbachawene amewapa pole familia ya marehemu na kueleza kuwa
katika kipindi chake cha ubunge Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai alitoa
mkubwa kama mbunge na kama mtaalamu wa Uchumi.
"Mheshimiwa
Rais anatoa pole nyingine kwenu familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki
wote walioguswa na msiba huu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake
lihimidiwe, Amina" Amesema Mheshimiwa
Simbachawene.
Mwili wa Marehemu
Christina Lissu Mughwai umesafirishwa leo kwenda kijiji cha Mahambe Mkoani Singida
kwa Mazishi.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
12 April, 2016
No comments:
Post a Comment