Header Ads

MWAKILISHI WHO ATEMBELEA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR KUPATA TARIFA ZA KIPINDUPINDU

Waziri wa Afya Mhe, Mahmoud Thabit Kombo kulia akisalimiana na Muakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO alioko Zanizbar Dk, Ghirmay Andemichael mara baada ya kuwasili Ofisini kwake Mnazi mmoja Mjini Zanzibar, kupata taarifa ya maradhi ya kipindupindu yalioanza mwezi Septemba mwaka jana hapa Zanzibar.
Waziri wa Afya Mhe, Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na muakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO nchini Tanzania Dk, Rufaro Chatora kushoto yake pamoja na ujumbe aliofuatana nao Ofisini kwake Mnazi mmoja Mjini Zanzibar. Muakilishi huyo alifika kuangalia hali ya maradhi ya kipindupindu Zanzibar.
Muakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO Dk, Rufaro Chatora katikati akizungumza na Wakuu wa sekta mbalimbali katika Wizara ya Afya Zanzibar kuhusiana na Maradhi ya Kipindupindu Zanzibar. Kushoto yake ni Muakilishi wa WHO aliopo Zanzibar Dk, Ghirmay Andemichael na kulia yake ni Katibu Mkuu wizara ya Afya Zanzibar Mohd Saleh Jidawi.

No comments:

Powered by Blogger.