MKURUGENZI WA HALMASHAURI ATAKAESHINDWA KUTENGA ASILIMIA KUMI KWA AJILI YA WANAWAKE NA VIJANA ATAONDOLEWA-WAZIRI MKUU
WAZIRI
Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Kassim Majaliwa
amesema Mkurugezi yeyote wa Halmashauri nchini atakayeshindwa kutenga
asilimia 10 ya mapato kwa ajili ya wanawake na vijana ataondolewa.
Amesema
suala la kila Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili
ya kuwawezesha wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi na kuondokana na
utegemezi ni la lazima na si hiari.Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo
leo (10 Aprili, 2016) alipokuwa anazungumza kwa nyakati tofauti na
wananchi wa vijiji vya Kitandi, Mtimbo, Likunja, Nkowe na Namahema
ambako lifanya mikutano ya hadhara.
“Halmashauri
ambayo itashindwa kutenga asilimia 10 kwa maana asilimia tano kwa ajili
ya vijana na tano kwa ajili ya akinamama Mkurugenzi wake atakuwa
anatafuta safariiri,” amesema Waziri Mkuu, Majaliwa.
Waziri
Mkuu, Majaliwa yupo wilayani Ruangwa, Lindi kwa ajili ya ziara ya
kikazi inayolenga kukagua shughuli za maendeleo, ambapo amewasisitiza
Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutimiza wajibu wao na serikali
haitamvumilia yeyote atakayeshindwa.
Pia
Waziri Mkuu, Majaliwa amewataka wananchi hao kujiunga katika vikundi
vya uzalishaji mali ili zitakapofika sh milioni 50 za kila kijiji
zilizoahidiwa na Rais, Dk. John Magufuli waweze kunufaika.Amesema fedha
hizo ambazo zitatolewa kuanzia mwezi Julai mwaka huu zitagawiwa katika
vikundi mbalimbali vilivyosajiliwa na si kwa mtu mmoja mmoja hivyo
amewataka watendaji wa kata na vijiji kuwahamasisha wananchi kujiunga
katika vikundi.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu, Majaliwa amesema serikali imefuta tozo tano
kati ya tisa za zao la korosho zilizokuwa kero ya muda mrefu na kufanya
wakulima wachukie mfumo wa Stakabadhi ghalani.
Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment