MH. ANNE KILANGO MALECELA AWAHUTUBIA WAKAZI WA SHINYANGA, ASIMIKWA KUWA CHIFU WA KISUKUMA
Hapa
ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambapo April 05, 2016
kumefanyika mkutano wa mkuu mpya wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Anne
Kilango Malecela amejitambulisha kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga na
kueleza vipaumbele vyake katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Mkutano
huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya
siasa,viongozi wa dini na kimila huku mamia ya wakazi wa Shinyanga
wakijitokeza kwa wingi kumsikiliza mkuu huyo wa mkoa. Akiwahutubia
wakazi wa Shinyanga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela
ambaye anakuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga wa 19 tangu nchi ipate uhuru na
mwanamke pekee kuongoza mkoa huo,amesema amekuja mkoani Shinyanga kwa
ajili ya kumsaidia rais John Pombe Magufuli kuwaletea maendeleo wananchi
kwa kutekeleza kauli mbiu ya Hapa Kazi tu.
Kilango
amesema atahakikisha tatizo la uhaba wa madawati katika shule za mkoa
wa Shinyanga linamalizika haraka iwezekanavyo huku akisisitiza nia yake
ya kutaka mkoa kushika nafasi ya kwanza mfululizo katika matokeo ya
mitihani mbalimbali kitaifa pamoja na kwamba tangu mwaka 2012 hadi 2015
mkoa umekuwa ukishika nafasi ya kwanza na ya pili katika matokeo ya
kidato cha nne.
Mkuu
huyo wa mkoa aliyepewa jina la Mbula amepongeza viongozi wa mkoa kwa
kupunguza kwa kiasi kikubwa mauaji ya vikongwe na albino na kuhamasisha
jamii kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati.Katika
hatua nyingine Kilango ambaye amekuwa mbunge kwa kipindi cha miaka
mitano amesema hatakuwa kiongozi wa kukaa ofisini na badala yake atakuwa
kiongozi anayewatembelea wananchi ili kutatua matatizo yao.
"Nitatenga
walau siku moja kila wiki kuwatembelea wananchi katika mitaa na
vijiji...watendaji wa serikali walioko chini yangu,nataka kuanzia leo
iwe mwisho kunyanyasa wananchi,naombeni msikilize kero zao badala ya
kuwapa majibu ya ovyo ovyo",ameeleza Kilango.
"Zile
shilingi milioni 50 alizoahidi mheshimiwa rais wakati wa kampeni za
uchaguzi zitaletwa,naomba mzitumie vizuri,nataka mkoa huu uwe wa mfano
kwa maendeleo,naombeni ushirikiano,naahidi kushirikiana kwa ukaribu pia
na viongozi wa dini,hawa ni watu muhimu sana",ameongeza Kilango Pamoja
na mambo mengine wazee wa kimila/machifu wa kabila la Kisukuma
wamesimika mheshimiwa Kilango kuwa chifu wa kisukama na wamemkabidhi
dhana mbalimbali za kimila mkuu huyo wa mkoa ili azitumie katika uongozi
wake kuwaongoza wananchi wa Shinyanga ambao wengi wao ni wasukuma.
Viongozi
hao wa kimila pia wamemtangaza mheshimiwa Anne Kilango Malecela kuwa
"Kanumba" maana yake mtendaji na msimamizi mkuu kwa mkoa na kumpa jina
la Kimila "Mbula" likiwa na maana ya mvua.
Mkuu
huyo wa mkoa pia ameombewa dua na viongozi wa dini waliohudhuria
mkutano huo ambao umefurahiwa na wakazi wengi wa mkoa wa Shinyanga
waliodai kuwa haijawahi kutokea mkuu wa mkoa akajitambulisha kwa
wananchi mara tu anapoteuliwa kushika nafasi hiyo.
"Mbula" ni jina kiongozi mkubwa wa kimila,Mbula alikuwa mganga wa 33 kati ya waganga 54 maarufu nchini Tanzania. Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio ametuletea picha 22 angalia hapa chiniMachifu
wa Kisukuma na wasaidizi wa machifu kutoka maeneo mbali mbali ya mkoa
wa Shinyanga wakijitambulisha kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa
Anne Kilango Malecela ambaye amepewa jina la "Mbula"Chifu
Charles Njange kutoka Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga(katikati)
akiwatambulisha viongozi wa kimila/machifu kutoka maeneo mbalimbali ya
mkoa wa Shinyanga ambao walitumia fursa hiyo kumkabidhi mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Anne Kilango Malecela(aliyesimama jukwaani kushoto) silaha za
kimila na mavazi ya kimila.
No comments:
Post a Comment