KUBENEA HAUKUMIA KIFUNGO CHA NJE
Mhe. Said Kubenea– Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA).
Na. Raymond Mushumbusi– Dar es salaam.
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saeed
Kubenea kifungo cha nje cha miezi mitatu kutokana kosa la kutumia lugha
ya matusi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda
ambaye sasa ni Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam.
Akisoma
hukumu hiyo leo Jijini Dar es Salaam Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu
Thomas Simba amesema kuwa mahakama imeamua kumpa mshitakiwa adhabu ya
kifungo hicho kwa kuwa ndilo kosa lake la kwanza, hivyo Mshatakiwa
anastahili kupata adhabu ya huruma.
Chini
ya adhabu hiyo iliyotolewa chini ya kifungu no 89 kifungo kidogo cha
kwanza Mhe. Kubenea hatakiwi kufanya kosa la aina yoyote ambalo
litamsababisha arudishwe tena mahakamani na endapo itatokea akafanya
hivyo mahakama itampa adhabu ya kifungo cha kwenda jela.
Awali
kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo mshtakiwa Said Kubenea mbele ya
Hakimu Mkazi Thomas Simba alipewa nafasi ya kujitetea ni kwanini
asipewe adhabu kali kwa kosa alilolitenda ambapo alieleza Mahakama hiyo
kuwa hakuwa na nia mbaya ya kwenda kufanya fujo eneo la tukio ambapo
kulikuwa na mgomo wa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha TOOKU cha
jijini Dar es salaam bali alikwenda kwa lengo la kutafuta suluhu ya
mgomo huo akiwa kama mwakilishi wa wananchi wa
jimbo la Ubungo.
Ikumbukwe
kuwa Jalada la kesi hiyo na 320 ya mwaka lilifunguliwa na Jamhuri dhidi
ya Said Kubenea kwa kosa la kutumia lugha ya matusi kwa aliyekuwa mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda, Aidha upande wa washtakiwa
wameonyesha kutoridhishwa na
hukumu hiyo na wameomba kukata rufaa.
No comments:
Post a Comment