JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAMKAMATA MTU MMOJA ALIYEKUTWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU AINA YA CHARGER.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA, MTU MMOJA MKAZI WA UYOLE JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA MASHAKA RAMADHAN [21] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA AKIWA NA KETE 12 ZA DAWA ZIDHANIWAZO ZA KULEVYA.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2016 MAJIRA YA SAA 10:20 ASUBUHI KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA HUKO ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA,
JIJI NA MKOA WA MBEYA. UPELELEZI NA UCHUNGUZI ZAIDI UNAENDELEA ILI
KUBAINI AINA YA DAWA HIZO.
KATIKA
MSAKO WA PILI: JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
MKAZI WA MATENKI – KASUMULU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PETER CHANGWA [21]
AKIWA NA POMBE HARAMU [GONGO] UJAZO WA LITA 20.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2016 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO ENEO
LA FORODHA –KASUMULU, KATA YA NGANA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA
KYELA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUWA AKISAFIRISHA POMBE HIYO HARAMU
KWENYE BAISKELI YAKE AKITOKEA MALAWI.
KATIKA
TUKIO LA TATU, MTU MMOJA MKAZI WA IGOGWE WILAYA YA RUNGWE MKOANI MBEYA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LESSA JAPHET [45] ANASHIKILIWA NA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI
CHUPA 24 AINA YA CHARGER.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 19.04.2016 MAJIRA YA
SAA 12:30 MCHANA HUKO ENEO LA MTAA WA IGOGWE, KATA YA KAWETELE, TARAFA
YA TUKUYU MJINI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.
SERIKALI
IMEPIGA MARUFUKU UINGIZAJI NA MATUMIZI YA POMBE HIZO KWANI NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI. POMBE HIZO NI PAMOJA NA CHARGER, RIDDER, DOUBLE
PUNCH, POWER NO.1 NA BWENZI AMBAZO UINGIZWA NCHINI KUTOKA NCHINI JIRANI
YA MALAWI.
WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI EMANUEL G.
LUKULA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE KALI NA POMBE
HARAMU [GONGO] KWANI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA
JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UINGIZAJI WA POMBE
KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI
YAO.
KATIKA
TUKIO LA NNE, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MHAMIAJI
HARAMU RAIA WA NCHINI KONGO AITWAYE JEAN MWELA [21] KWA KOSA LA KUINGIA
NCHINI BILA KIBALI.
MHAMIAJI
HUYO ALIKAMATWA NA ASKARI WALIOKUWA DORIA MNAMO TAREHE 19.04.2016
MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO ENEO LA UZUNGUNI – ROMAN KATOLIKI, KATA
NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMKABIDHI
IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.
Imesainiwa na:
[EMANUEL G.LUKULA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Namba ya Simu: 0658 376 006 – Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.
No comments:
Post a Comment