GSM WASAIDI KITENGO CHA MOI KUWEKA KAMBI YA OPARESHENI YA WATOTO WENYE MGONGO WAZI NA WENYE VICHWA VIKUBWA.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI
imesema kuanzisha kambi za kufanya oparesheni kwa watoto wenye migongo
wazi na vichwa vikubwa itasaidia kuokoa maisha ya watoto hao kutokana
na wazazi wao kushindwa kumudu gharama za oparesheni hizo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati makababidhiano ya
magari kwa ajili ya kambi hizo, Mwakilishi wa Waziri wa Afya na
Maendeleo jamii jinsia, Watoto , Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda
amesema kuwa Mfuko wa GSM wametambua matatizo ya watoto hao na kuamua
kutoa sehemu yao katika kuhakikisha watoto hao wanafanyiwa oparesheni.
Makonda
amesema kambi hizo wazazi watapeleka watoto tu ambayo ndio gharama yab
kufanya watoto wao wafanyiwe oparesheni ya matatizo yao.
Amesema
kuwa watu walikuwa wanafikiria ndani ya bajeti tu bila kuangalia wadau
wana uwezo gani na kusababisha mambo kurudi nyuma kwa GMS wameonyesha
njia katika kufanya ufadhili wa oparesheni hiyo.
‘’Naamini
watoto hao watakuwa kuwa watumishi wenye maadili kutokana na matatizo
waliopata na watu wengine wakahangaikia hivyo hawawezi kuwa mafisadi kwa
kujua atachochukua kuna watu wanahitaji’’amesema Makonda.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk.Othman Kiloloma amesema kuwa daktari
wenye utaalamu huo ni daktari tisa tu kati ya hao nane ni Hospitali ya
Taifa Muhimbili na mmoja Hospitali ya Bungando.
Dk.Kiloloma
amesema kufanya operesheni ya mtoto mmoja ni sh. Laki saba hadi milioni
moja ambapo baadhi wanashindwa kumudu hivyo ufadhili wa GSM utafanya
kuweka kambi na kutoa huduma hiyo bure kwa watoto pamoja na kutoa elimu
kwa baadhi ya daktari juu ya oparesheni ya watoto wenye migongo wazi na
vichwa vikubwa.
Afisa
Mawasiliano wa GSM , AKhalfan Kiwamba amesema kuwa wanatambua matatizo
ya watoto hao na kuamua kufanya ufadhili ili waweze kufanyiwa
oparesheni hiyo.
Amesema
kambi hizo awamu ya kwanza itakuwa Mkoa wa Mwanza Aprili 27 hadi 30,
Shinyanga Mei 2 hadi 4, Singida Mei 6 hadi 8, Dodoma 10 hadi 13,
Morogoro Mei 15 hadi 17 .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata na
utepe kuzindua magari ambayo yametolewa na Mfuko wa GSM kwaajili ya
kusidia kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa pamoja na
watoto wenye migongo wazi katika kambi itakayofanyika katika mikoa ya Mwanza
Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka
Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa
kambi ya upasuaji ya watoto wa wenye vichwa vikubwa na watoto wenye
matatizo ya mgongo wazi ambapo Mfuko wa GMS kushirikiana na Taasisi ya
Mifupa (MOI) katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili wataanza kambi hiyo
katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka
4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15
mpaka 17. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba
na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma na Mkurugenzi wa tiba MOI
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Samwel Swai.
Daktari
Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili,
Othman Kiloloma katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam leo kuhusiana na kambi ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa
vikubwa na watoto wenye Migongo wazi. Kulia ni kuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
Afisa
Uhusiano wa Mfuko wa GSM, Khalfan Kiwamba akizumgumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na GSM kutoa mchango wake kwa
kusaidia watoto wenye matatizo ya Mgongo wazi na watoto wenye vichwa
vikubwa. Kusoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
No comments:
Post a Comment