TUSHIRIKIANE KUTOKOMEZA UKEKETAJI KWA WATOTO WA KIKE-UMMY MWALIMU
Mhe. Waziri wa Afya.Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumzia uzefu wa Tanzania
katika kukabiliana na tatizo la ukeketaji akiwa na wazungumzaji wengine
katika Meza Kuu, kutoka kushoto ni Mke wa Rais wa Burkina Faso Bi.
Sika Bella Kabore, Bw. Benoit Kalasi (UNFPA), Bi.Emma Bonino Waziri wa
zamani wa Mambo ya Nje Italia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma
za Jamii, Mhe. Peter Serukamba akifuatilia majadiliano kuhusu tatizo la
ukeketaji na adhari zake wa afya na maendeleo ya mtoto wa kike na
mwanamke.
Wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi nao wakifuatilia majadiliano
yaliyovutia washiriki wengi kuhusu madhara yatokanayo na ukeketaji na
namna gani jamii inatakiwa kushirikiana kutokoza tatizo hilo.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano na majadiliano kuhusu utokomezaji wa
vitendo vya ukeketaji na uhusiano wake na utekelezaji wa Malengo ya
Maendeleo Endelevu. Mkutano huu uliandaliwa kwa pamoja na Wakilishi za
Kudumu za Tanzania, Burkina Faso, Italy, Iran, UNFPA na UNCEF.
Mhe Waziri Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na washiriki wa majadiliano kuhusu ukeketaji.
Waziri Mwalimu akibadilishana mawazo na Waziri mwenzie Sicily Kariuki kutoka Kenya
Na Mwandishi Maalum, New York
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ( Mb) amesisitiza
kuwa ni kwa ushirikiano baina ya Serikali na
jamii ndipo tatizo la ukeketaji
kwa watoto wa kike na wanawake litakapoweza kutokomezwa.
Akaongeza
kwamba, serikali inaweza kutunga sheria nyingi za kukabiliana na
tatizo hilo lakini kama jamii yenyewe kuanzia ngazi
ya familia isipotoa ushuriano wa dhani itachukua muda mrefu kwa tatizo
hilo kutokomezwa. Alikuwa akizungumza wakati wa
majadiliano ya mkutano wa kuhusu utokomezwaji
vitendo vya ukeketaji kama sehemu
muhimu ya utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( Agenda
2030.
Waziri Ummy Mwalimu alikuwa mmoja
wa wazungumzaji wakuu katika
mkutano huo uliowahusisha
Mke wa Rais wa Burkina Faso,
Bibi. Sika Bella Kabore, Mawaziri na
Asasi za Kiraia na uliandaliwa kwa pamoja na Wakilishi za kudumu za Tanzania, Italy, Iran, Burkina Faso,UNFPA na UNICEF,
ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni
ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake.
Na kwa sababu hiyo, Waziri Ummy Mwalimu, amerejea kutoa wito kwa
watanzania wote kwa katika ujumla wao wakiwamo wazee wa kimila, viongozi wa dini na
vijana wakiume kutoa ushirikiano
kwa serikali na wadau wengine ili
hatimaye tatizo hilo ambalo
linaelezwa kuwa siyo tu lina madhara makubwa kiafya na
kisaikolojia lakini pia ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
No comments:
Post a Comment