MADAM SOPHY CHARITY EVENTS YAZINDULIWA RASMI, JAMII YATAKIWA KUSAIDIA WENYE UHITAJI MAALUM
Baadhi
ya wadau wakitoa zawadi na vitu mbalimbali kwa Madam Sophy ambavyo
vitagawiwa kwa wanafunzi wa shule hiyo ya Jeshi la Wokovu na wale wa
Makumbusho Sekondari.
Wanafunzi wenye ulemavu wa viungo na ngozi wakiwa katika tukio hilo.
Wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wakitoa burudani kwa mgeni rasmi (hayupo pichani).
Taasisi
mpya ya Kijamii ijulikanayo Madam Sophy Charity Events yenye malengo ya
kusaidia jamii hasa ile yenye uhitaji maalum ikiwemo watu wasiojiweza
imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam sambamba na
kutoa misaada mbalimbali kwa watu na watoto wenye uhitaji huo maalum.
Tukio
hilo la kipekee lililoandaliwa na kuratibiwa na Mwanadada, Sophia
Mbeyela pia lilijumuisha wadau na marafiki mbalimbali walioungana na
Madam Sophy katika kufanikisha tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa
shule ya Msingi ya Jeshi la Wokovu ambayo ilishirikisha watoto
wanafunzi wa kituo cha Matumaini wenye Ulemavu wa viungo na ngozi.
Madam
Sophy na marafiki zake kwa pamoja waliweza kutoa misaada ya vitu
mbalimbali kwa watoto hao ambapo pia walipata wasaha wa kuzindua taasisi
hiyo huku mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Masauni ambaye aliwakilishwa na Mbunge Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul
Jumaa ambaye aliahidi kufikisha kilio cha walemavu na watu wenye
mahitaji maalum Serikalini paamoja na kwenda kuwasilisha Bungeni
ilikuona utekelezaji wake kwa ukaribu.
“Madam
Sophy Charity. ni taasisi ambayo zaidi ni kuona wenzetu wenye uhitaji
maalum hasa walemavu wanapata nafuu katika kuendana na majukumu ya nchi
hii kwani sote tuna haki sawa kama wengine na ulemavu wetu
usitutenganishe. Tunahitaji Serikali kuhakikisha inashusha bei vifaa
vyote vya walemavu ikwemo viungo vya bandia ikiwemo mikono na miguu
ambayo kwa kiungo mimoja pekee yake kinakaribia hadi milioni moja”
alieleza Madam Sophy.
Madam
Sophy aliongeza kuwa, Serikali inayo wajibu wa kujenga shule nyingi
zaidi za watu wenye ulemavu kwani zilizopo sasa bado ni chache na watu
wenye ulemavu wamehamasika kujitokeza kusoma hivyo jukumu lililopo ni
kuhakikisha wanaongeza shule za watu hao pamoja na kutengeneza
miundombinu ambayo inakuwa rafiki kwa walemavu kuanzia mashuleni na hata
maeneo muhimu.
Aidha,
Kwa upande wake, mgeni rasmi huyo aliweza kuchangia kiasi cha Sh Laki
tano kwa ajili ya kuunga mkono juhudi na harakati za Madam Sophy ambapo
alieleza kuwa, licha ya ulemvu wake ameweza kuonesha njia ya kujikwamua
pamoja na kuwasaidia wenzake.
Madam
Sophy ambaye kitaaluma ni Mwalimu, ni miongoni mwa wanafunzi waliopata
kusoma katika shule hiyo na kumaliza hapo darasa la saba mwaka 2002
ambapo pia aliendelea na shule mbalimbali ikiwemo Sekondari ya Jangwani
na baadae chuo, ameomba wadau kujitokeza kuungana naye katika
kuhakikisha wanasaidia watu na jamii yenye uhitaji maalum kwani kutoa ni
moyo.
No comments:
Post a Comment