CCM YATAKA WAKURUGENZI MANISPAA YA ILALA, KINONDONI WAWAJIBISHWE KUCHELEWESHA UCHAGUZI WA MEYA JIJINI DAR ES SALAAM
Na Dotto Mwaibale
CHAMA
cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam kimemuomba Waziri Ofisi ya Rais
,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Utumishi na Utawala
Bora, George Simbachawene kuwawajibisha Wakurugenzi wa Manispaa ya Ilala
na Kinondoni kwa kile walichodai ni kuvuruga uchaguzi wa Meya wa Jiji
la Dar es Salaam.
Hayo
yalizungumzwa Dar es Salaam jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Mkoa wa Dar e Salaam, Juma Simba 'Gadafi' wakati akizungumza na
waandishi wa habari ambapo alisema kumekuwa na sintofahamu hadi sasa
kuhusiana na uchaguzi huo kutokana na woga wa wakurugenzi hao ambao
wameshindwa kujiamini.
"
Wakurugenzi hawa ndiyo chanzo cha vurugu katika uchaguzi huu wa meya
tumewaomba wakurugenzi hawa watoe tamko na tafsri sahihi ya ushiriki kwa
wajumbe wenye sifa ili kuacha kuupotosha umma juu ya uchaguzi
huu,"alisema Gadafi.
Gadafi
alisema kuwa wakurugenzi hao kwa makusudi na huku wakifahamu wanakiuka
sheria waliruhusu baadhi ya maswahiba wao kutoka chama cha upinzani (
Ukawa) ambao walitoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam kuingia kwenye
uchaguzi uliovurugika.
Gadafi
alisema mwanachama yeyote wa CCM anaruhusiwa kufanya uchaguzi katika
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kupingwa kama taratibu
unavyoelekeza.
Alisema
hizi kauli zinazotolewa kuwa haiwezekani wajumbe wakatoka nje ya Dar es
Salaam na kupiga kula eneo lingine hazina ukweli wowote kwani siku za
nyuma ziliwahi kufanyika kwa vyama vingine lakini hakukuwa na
kulalamika.
Aidha
katika hatua nyingine Simba amesema Meya wa Ukawa walioshinda katika
Manispaa za Kinondoni na Ilala wanatakiwa watambue kuwa Halmshauri hizo
hazitaendeshwa kwa ilani ya chama chao bali ni ilani ya Chama Cha
Mapinduzi kwa kuwa asilimia 60 ya bajeti ya maendeleo inaongozwa na
chama.
No comments:
Post a Comment