WITO UMETOLEWA KWA WAMILIKI WA SILAHA KUHAKIKI SILAHA ZAO KWA WAKATI
Pichani :Kamanda Liberatus Sabas, alipokuwa akifunga Kampeni za ABIRIA PAZA SAUTI, Jijini Arusha,
Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Arusha.
Jeshi
la polisi mkoa wa Arusha limewataka watu wote wanaomiliki silaha kwa
njia halali wafike kwenye kituo cha polisi kuhakiki silaha zao na
kuzilipia kama inavyostahili na kwa kufuata utaratibu kama sheria
inavyoagiza.
Hayo
ya mesemwa Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, kwamba kila
mwaka huwa kila mwenye silaha anafika polisi na silaha yake na vitabu
vyake kwaajili ya kuihahiki na kuilipia kama inavyostahili ,na kama zipo
tuhuma zozote kutokana na matumizi ya silaha, itasimamishwa kwaajili ya
taratibu zingine na kunyang’anywa hadi hapo jeshi litakapojiridhisha
kuwa silaha hiyo matumizi yake ni sahihi ama siyo sahihi Kamanda amesema
utaratibu huu huwa unaratibiwa na makao makuu ya jeshi la polisi
kwaajili ya kuhakiki silaha ,ikiwa ni pamoja na kulipia mapato ya
serikali ,amewataka watu wanaomiliki silaha wafuate masharti yake kama
inavyotakiwa, nawakumbuke sheria inambana kila mtu mara anapotenda kosa
,na kama mtu akiitumia ndivyosivyo atanyang’anywa silaha kwa kutumia
sheria iliyowekwa.
Ameongeza
kuwa wapo watu ambao wamewatishia silaha wenzao,na wengine kesi zao
zipo tayari na zingine zimefutiwa umiliki kwa mujibu wa sheria, amesema
kimsingi kabla mtu hajakabidhiwa silaha ili amiliki, yapo masharti
yakufuata na yapo kwenye kitabu kile cha leseni anachopewa wakati wa
umiliki, amesema kuwa ukitoka nje ya hayo masharti huna sifa ya kumiliki
silaha.
Kamanda
Sabas ametoa anagalizo kwa wamiliki wa silaha na kusema kuwu silaha ya
moto siyo kama panga,silaha hiyo ukiifanyia kosa mara moja yaweza kuua
mtu au watu hivyo amewataka kuwa makini sana katika ufuatiliaji wa
umiliki, pamoja na namna zinavyotunzwa,amesema jeshi la polisi lipo
makini kufuatilia kwa ukaribu wakithibitisha silaha haitunzwi kama
inavyostahili utanyang’anywa.aidha amesema kwa wazee amabao umri wao
umeenda nab ado wanamiliki silaha huwa wanaichukua na kuihifadhi .
Amehitimisha
kwa kusema kuwa kila , mtu amnayetaka kumiliki silaha, kamati za ulinzi
na usalama kuanzia kwenye kata ,Wilaya, Mkoa wakamuidhinisha kuwa na
silaha afuate masharti na kuitunza silaha isije ikaangukia kwenye mikono
ya wahalifu wakaitumia isivyo halali sheria itafuata mkondo wake,
Silaha huwa zinatakiwa kulipiwa kila mwaka kuanzia mwezi julai hadi
septemba ukichelewa kulipia unapigwa penati kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment