Waziri Ummy apokea vifaa katika wodi ya Afya ya Uzazi ya Mama na Mtoto Muhimbili
Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu
akipokea vifaa kutoka kwa Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa yaTaifa Lauren
Rugambwa Bwanakunu vitakavyotumika katika wodi ya Afya ya uzazi ya Mama
na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wa pili kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi Hospitali ya Muhimbili Prof Lawerence Mseru na nayefata ni
katibu Mkuu wa wizara hiyo Mpoki Ulisubisya .
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu
amepokea vifaa vitakavyotumika katika wodi ya Afya ya uzazi ya Mama na
Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni agizo la Mhe.Rais
alililolitoa mapema mwishoni wa wiki iliyopita katika kuhakikisha kuwa
wakinamama wanaojifungua hawalali chini.
Akipokea
vifaa hivyo Mhe. Ummy Mwalimu amesema anamshukuru sana Mhe Rais kwa
kuona changamoto hii ya wakina mama kulala chini wakati wakitoka
kujifungua na kumuahidi Mhe. Rais kusilimamia vyema suala hilo na
kuwaagiza wakurugenzi husika kumpa taarifa ya kuhusu vitanda na magodoro
katika Hospitali zote zilizo chini ya wizara yake.
“
Kuanzia sasa sitolala na natuma salamu kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwa
fursa hii ni wajibu wao kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya afaya hasa
katika vifaa hususan vitanda na magodoro ili kupunguza tatizo hili la
wagonjwa katika Hospitali zetu kulala chini wakati tuna uwezo wa kupata
vitanda na magodoro”
‘”Mhe.Rais
amenifundisha na ametufundisha sote kwamba kutatua jambo sio mpaka
mkae vikao au semina ili kujadili ila inawezekana kama mkiweka nia ya
kulifanya jambo hilo na kuachana na zile kauli za tunalifanyia kazi,
tupo katika michakato na kauli kama hizo zisizotatua tatizo kwa wakati
unaotakiwa”alisema Ummy.
Bohari
ya Dawa ya Taifa imekabidhi jumla ya vitanda 120, Magodoro 120, Mashuka
480, vitanda vya kuzalishia 10,vitanda 10 vya kulaza watoto ambao
hawajatimia Njiti na jumla ya vifaa vyote vina thamani ya shilling
Million 100.
Uaandaaji
wa wodi hiyo ya akimama wanaojifungua katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili umekuja baada ya agizo la Mhe.Rais Dkt John Pombe Magufuli
alilolitoa hivi karibuni alipokuwa akiongea na wazee wa Mkoa wa Dar es
Salam na kutoa siku mbili kwa wizara Ya Afya kuhamisha ofisi
zilizokuwepo za kitengo Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto na kuifanya kuwa
wodi ya akina mama ili kupunguza tatizo la kulala chini kwa akina mama
wanaotoka kujifungua.
No comments:
Post a Comment