WAKURUGENZI WANNE WA MSD WASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA UBADHIRIFU WA FEDHA
Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu
amewasimamisha wakurugenzi toka Bohari ya Dawa ya Taifa(MSD) kwa
ubadhilifu wa fedha takribani Shillingi Billion 1.5.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto baada ya kupokea vifaa
toka Bohari Kuu ya Dawa ya Taifa (MSD) amesema amepata taarifa ya
uchunguzi ofisini kwake ya ubadhilifu wa kiasi hicho cha fedha na kuamua
kuwasimamisha wakurugenzi wanne kupisha uchunguzi.
“
Nimeletewa taarifa ofisini kwangu na nimeamua kuchukua fursa hii
kuwaambia na hili pia kwamba nimewasimamisha wakurugenzi wanne toka
Bohari ya Kuu Dawa ya Taifa kwa ubadhilifu wa fedha na nisingeweza
kusubiri nitumbuliwe mimi jipu na Mhe.Rais kwahiyo nimeamua kuwachukulia hatua kwa kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi”
“
Hizi ni zama za kufanya kazi na kuwajibika sasa inabidi tuwajibike kwa
kufanya kazi na hatutowavumilia watendaji watakaoenda kinyume na
utaratibu katika ofisi yoyote ile katika sekta ya afya na tutawachukulia
hatua kwani tunataka uwajibikaji ili kuiendeleza sekta ya afya ambayo ni muhimu sana kwa kila mwanadamu” Alisema Ummy.
Amewataja
aliowasimamisha kazi kuwa ni Joseph Tesha Mkurugenzi wa Fedha na
Mipango, Misanga Muja Mkurugenzi wa Ugavi, Heri Mchunga Mkurugenzi wa
Manunuzi na Cosmas Mwaifani Mkurugenzi Kanda na Huduma kwa Wateja ambapo
amewataka Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari ya Dawa ya Taifa
kuwaandikia barua mara moja ya kuwasimamisha kazi.
Katika
kuboresha sekta ya afya nchini Wizara wa Afya ,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee imejipanga kufanya kazi kwa taratibu na
misingi iliyopo ili kuhakikisha inapeleka mbele gurudumu la maendeleo ya
hasa katika sekta ya afya kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment