WAZIRI MBARAWA ATAKA MAKANDARASI KUTOA MIKATABA YA AJIRA
Mkandarasi
wa SynoHydo Corporation Ltd akimkabidhi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa
barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa Km. 43.65 inaojengwa kwa
kiwango cha lami
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimuagiza
Mkandarasi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan
International Corporation Group Ltd (hayupo pichani) kuwapa mikataba
bora ya kazi wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo (wanaomsikiliza).
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza
jambo kwa Mkandarasi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya
China Henan International Corporation Group Ltd (pichani) kuwapa
mikataba bora ya kazi wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati)
akiagiza kuwekwa lami juu ya Daraja la Kola Wilayani Kondoa mkoani
Dodoma ili kuanza kupitika na kupunguza usumbufu wa magari wakati wa
mvua. (kushoto) ni Meneja ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga (Km.88.8)
Eng. Stone Cheng na (Kulia) ni Mhandisi Mshauri wa barabara hiyo.
Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu
akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.
Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) kuhusu hatua ya ujenzi iliyofikiwa
katika barabara ya Mela-Bonga (Km. 88.8) inayojengwa kwa kiwango cha
lami, (Wa pili kulia) ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Godfrey
Kombe na (wa kwanza kushoto) ni Eng. Deusdedit Kakoko kutoka TANROADS
makao makuu.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya Km. 43.65 ambao ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika kwa asilimia 80.
Kazi
ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela yenye urefu wa Km. 99.35
ukiendelea.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment