JAJI MKUU WA TANZANIA MHE.OTHMAN CHANDE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI.
Watumishi
wa Mahakama ya Tanzania na wadau mbalimbali wa wakiingia katika viwanja
vya Mnazi mmoja kwa maandamano leo jijini Dar es salaam wakati wa
Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.
Watumishi
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Askari
wa Jeshi la Magereza na Watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka
(DPP) wakiwa wamebeba mabango ya Ofisi zao wakati wa Ufunguzi wa
maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini leo jijini Dar es salaam.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (Mwenye T-shirt nyeupe kulia), Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki (wa Pili kulia) na Watendaji
wa Mahakama ya Tanzania wakishiriki mazoezi ya viungo ya pamoja na wadau
mbalimbali wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa
Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini.
Jaji
Kiongozi Mhe. Shaban Lila (katikati) akiongoza mazoezi ya pamoja ya
Wadau wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
salaam wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria nchini.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akizungumza na wadau mbalimbali wa
Mahakama waliohudhuria Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka
2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.
No comments:
Post a Comment