WAZIRI ANNASTAZIA WAMBURA ATEMBELEA TFF.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura
akipokeza zawadi ya jezi ya timu ya Taifa ya Tanzania kutoka kwa Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji , Said Mohamed.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia
Wamburaakizungumza na viongozi na wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake
"Twiga stars" leo alipotembelea TFF.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura leo
ametembela ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na
kupata kujionea shughuli mbalimbali zinazondeshwa na shirikiso hilo.
Akiongea
na viongozi na wachezaji wa timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars”
waliopo kambini kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za
Mataifa Afrika kwa Wanawake dhidi ya Zimbambwe, Wambura amesema Serikali
itashirikiana na TFF kuhakikisha timu inapata ushindi katika mchezo huo
wa awali utakaochezwa Machi 4, 2016.
Wambura
amewataka wachezaji wa Twiga Stars kuwa na nidhamu ndani na nje ya
uwanja, kujituma na kuiipenda kazi yao hiyo ambayo kwa sasa ni ajira
itakayoweza kuwasaidia kuendesha maisha yao.
Aidha
Wambura amesema anaamini kuwa Twiga Stara bado wana nafasi ya kufanya
vizuri katika mchezo unaowakbalili, na kuwaomba kupambana zaidi
kuhakikisha inapanda na kushinda nafasi ya kwanza Afrika katika soka la
wanawake.
Pia
amesema wizara yake inashugulikia maombi ya TFF kuiomba wizara ya
TAMISEMI ikasimishe mchezo wa mpira wa miguu katika mashindano ya
UMITASHUMITA na UMISSETA yaweze kusimamiwa na TFF kwani wao ndio wenye
utaalamu wa mchezo huu.
No comments:
Post a Comment