WATANZANIA WAMETAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA TAMASHA LA AMSHA MAMA TANZANIA.
WATANZANIA
wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la ‘Amsha Mama Tanzania’
linalotarajiwa kufanyika Machi 5 katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke
jijini Dar es Salaam .
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Kampuni
ya Candy record yenye makao Mkuu yake nchini Kenya ambao ndio waandaaji
wa tamasha hilo Joe Kariuki amesema wameamua kuleta tamasha nchini ili
kuwapa fursa akina mama wa Tanzania kujiinua kiuchumi .
“
Akina mama mjitokeze kwa wingi katika tamasha hili mahususi kwenu kwa
kuwa mtapata fursa mbalimbali na mtaweza kupata mambo mbalimbali ikiwemo
elimu” .Alisema Kariuki.
Kwa
upande wake balozi wa Amsha Mama nchini Khalid Ramadhani (Tundaman),
amewaomba wakinamama wachangamkie fursa kwani watajifunza mambo mengi
“Nawaomba
Mama zangu mjitokeze kwa wingi kwani tumepata bahati ya pekee ya
kupendelewa kuletewa tamasha nchini kwani ni adimu kutokea,” .alisema Tundaman.
Tamasha
hilo linatarajiwa kufanyika pia katika uwanja wa Ranchi ya Kedong
uliopo jiji la Naivasha nchini Kenya marchi 25-27 huku likitarajia
kukutanisha akinamama kutoka nchi zote za Afrika .
Aidha
kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii kama vile Juma Kassim ‘’Juma
Nature’’, Khadija Kopa, Roma Mkatoliki, Young Killer, Msagasumu, Man
fungo,Sharo mwamba,Q-Chief,Mr Blue,Snura,Tundaman,na Ally Choki.
Tamasha
la Amsha Mama linatarajiwa kukutanisha akinamama mbalimbali kwa lengo
la kujifunza kuhusu kujikwamua kiuchumi kwani wao ndio chachu ya
mafanikio.
Alisema
wamejipanga kuwapa radha tofauti watoto wa temeke na majirani zake
,hasa kwa akina mama kupata fursa ya kujielewa na kujitambua hasa katika
kuendeleza familia zao.
No comments:
Post a Comment