Vyama vya Siasa Nchini Vyatakiwa Kuheshimu Katiba na Kanuni Zake
Msajili
wa Vyama vya Siasa Nchini Mhe. JaJi Francis S.K. Mutungi amevitaka
vyama vya Siasa nchini kuhakikisha kuwa Katiba na Kanuni za Vyama vya
Siasa zinaheshimiwa na kufuatwa katika utendaji wa kila siku wa chama
cha siasa ili kuepuka migogoro na migongano ndani ya vyama. Hayo
ameyabainisha kwenye barua yenye Kumb. Na. HA.322/362/01/103
aliyoiandikia vyama vya siasa mapema leo.
“Nimeona
ni vyema nitumie fursa hii kuviasa Vyama vya Siasa kuhusu hali hii,
kwani hali hii ya kufanya mambo kiholela pasipo kufuata Katiba na Kanuni
kama itaachwa iendelee hivi ndani ya vyama kwa hakika italeta migogoro
na mipasuko mikubwa ndani ya Vyama vya Siasa husika.”
“Wakati huu ambapo nchi yetu inasubiri marudio ya Uchaguzi Mkuu wa
Zanzibar, nimeandikiwa barua na pia kupata nakala za barua kutoka kwa
baadhi ya Vyama vya Siasa kuhusu migongano ya wanachama na viongozi au
viongozi wenyewe kwa wenyewe kuhusu suala la kushiriki uchaguzi wa
marudio Zanzibar. “alisema Jaji Mutungi
Barua hiyo ilibainisha kuwa suala hilo la migongano limejitokeza pia
kwa wingi kwenye Vyombo vya Habari, ambapo wanachama na viongozi au
viongozi wenyewe kwa wenyewe wametofautiana na kupingana hadharani.
Jaji
Mutungi amesema kwa mujibu wa Kanuni ya 3(1) ya kanuni za Usajili wa
Vyama vya Siasa za mwaka 1992 (GN.No. 111) Vyama vya Siasa
vinaposajiliwa vinapaswa kuwasilisha Katiba na Kanuni zake kwa Msajili
wa Vyama vya Siasa.
“Ikumbukwe
kwamba, suala la msingi hapa ni kwamba,sharti la kuwepo kwa Katiba na
Kanuni katika chama, kimsingi ni mwendelezo wa kukuza na kudumisha dhana
ya kuendesha Vyama kitaasisi kulingana na mwongozo uliokubalika na
kuasisiwa kichama kwa mfumo wa Katiba na Kanuni za chama na si kuendesha
chama kiholela kama inavyoelekea kuota mizizi kwa baadhi ya Vyama vya
Siasa hivi sasa.”ameongeza Jaji Mutungi
Jaji
Mutungi amevisihi Vyama vyote vya Siasa, kuhakikisha kwamba matamko ya
chama hususan yahusuyo msimamo wa chama kuhusu jambo zito la kisera,
kitaifa n.k., mathalan kama lilivyo la uchaguzi huu wa Zanzibar basi
yatolewe rasmi na mtu mwenye mamlaka ya kuongea kwa niaba ya chama. Na
endapo kuna mwananchama au kiongozi ambaye ataenda kinyume achukuliwe
hatua haraka iwezekanavyo na chama husika kwa kuzingatia katiba na
kanuni zake ili kuepusha sitofahamu inayokuwa imejitokeza katika jamii.
“Ni vyema
misimamo kama hiyo ya chama itokane pia na vikao halali vya chama na
siyo matakwa ya kiongozi mmoja au mwanachama mmoja au wachache.
Vinginevyo kama tutapeleka na kufanya uendeshaji wa vyama kiholela
tutachangia kuwachanganya wananchi na kupoteza kabisa imani na heshima
ya Jamii iliyokuwa imeanza kujengeka kwa Vyama vya Siasa”. Amesisitiza
Jaji Mutungi
Aidha
vyama vvya Siasa vimeaswa kuchua hatua ya haraka iwezekanavyo kwa
mwanachama au kiongozi wa chama anayefanya mawasiliano ama kutoa
matamko bila idhini ya mamlaka na pia vyama vimeonywa kutowajengea
wananchi tashwira ya kwamba kuna makundi yanagombania madaraka na
kuendeleza maslahi binafsi kwa sababu jambo hilo linashusha hadhi ya
vyama vya Siasa nchini.
No comments:
Post a Comment