SHIRIKA LA KIMATAIFA LA DKT INTERNATIONAL LAZINDUA “FIESTA CONDOMS” NCHINI TANZANIA
Wanandoa
mbalimbali wakishiriki kwenye michezo inayohamasiha upendo na
mshikamano wakati wa maandalizi ya kusherekea siku ya wapendano ambayo
iliambatana na uzinduzi rasmi wa chapa mpya za “Fiesta condoms” nchini
Tanzania. Uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ledger
Plaza, Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Mkurungezi
wa shirika la DKT International Tanzania Raphael Da Silva akizungumza
machache kwenye uzinduzi wa chapa mpya ya shirika hilo “Fiesta condoms”
katika soko la Tanzania uliofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ledger
Plaza, Kunduchi jijini Dar es salaam.
Meneja
Masoko wa shirika la DKT International Tanzania Bw. Davis Kambi
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa wa
uzinduzi rasmi wa “Fiesta condoms” nchini Tanzania uliofanyika hoteli ya
kitalii ya Ledger Plaza, Kunduchi jijini Dar es salaam mwishoni mwa
juma.
Meneja
Masoko wa shirika la DKT International Tanzania Bw. Davis Kambi
(Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa bahati nasibu
iliyochezeshwa na shirika hilo wakati wa uzinduzi wa “Fiesta condoms”
nchini Tanzania uliofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ledger Plaza
jijini Dar es salaam. Washindi hao walijishindia safari za mapumziko
kuelekea Zanzibar, Cape town na Dubai.
No comments:
Post a Comment