UJUMBE WA BENKI YA DUNIA WATEMBELEA MAONESHO YA WIKI YA SHERIA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.
Mtendaji
Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (kulia) akitoa ufafanuzi kwa
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird
aliyetembelea Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo, Katikati ni Afisa Mwandamizi
wa Masuala ya Kisekta wa Benki ya Dunia Bw. Waleed Maliki.
Mtendaji
Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (katikati) akimfafanulia jambo
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (kushoto)
alipotembelea banda la maonesho la Idara ya Malalamiko na Maadili la
Mahakama katika viwanja vya Mnazi Mmmoja leo.
Mtendaji
Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (kushoto) akionesha ugeni kutoka
Benki ya Dunia nchini Tanzania michoro ya majengo mapya ya Mahakama
yanayoendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini . Kutoka kulia ni
Bw. Larbi George Addo kutoka Benki ya Dunia akifuatiwa na Mkurugenzi wa
Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (wa pili kutoka kulia) na
Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Kisekta wa Benki hiyo Bw. Waleed
Maliki.
No comments:
Post a Comment