NDANI YA TAKUKURU KUNA ‘MAJIPU’ –KAIRUKI.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola akizungumza na
viongozi wa TAKUKURU katika mkutano wa kazi na viongozi hao uliofanyika
makuu ya ofisi hiyo mapema leo. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
– Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akimsikiliza kwa
umakini.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki
(Mb) akifungua mkutano wa kazi wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika makuu
ya ofisi hiyo mapema leo.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
aziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki
(Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wakaguzi wa kanda wa TAKUKURU mara
baada ya kufungua mkutano wa kazi wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika
makuu ya ofisi hiyo mapema leo.
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi Rais Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amesema
kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ina baadhi ya
watendaji wametumia nafasi zao vibaya na kufanya chombo hicho kukosa
uaminifu hivyo na kufanya chombo hicho kuwa na ‘majipu’ ambayo
yanatakiwa kupasuliwa.
Angela
ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa utendaji kazi
wa Takukuru uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, amesema chombo hicho
ni muhimu lakini kuna baadhi wametumia nafasi zao vibaya katika kufanya
kazi na taarifa anazo hivyo atashughulikia ikiwemo na kuandika kiapo cha
mali zao na kama walifanya warudie kujiridhisha.
Amesema
kuwa Takukuru inatakiwa kufika wilayani na mikoani kutokana na fedha
nyingi za miradi ya serikali zinakwenda huko ambapo ameutaja mkoa wa
Kilimanjaro unawatendaji ambao wametumia madaraka vibaya wa ubadhirifu
wa fedha za serikali hivyo Takukuru lazima ichukue hatua dhidi yao.
Amesema
kuwa ikitokea kuwepo na kutowajibika kwa chombo hicho serikali iamweza
kuwandoa wote kutokana na kuwepo kwa watu wenye sifa wa kufanya kazi
hiyo.
Aliongeza
kuwa katika Takukuru inatakiwa kujiridhisha na uchunguzi na sio kuwa
idadi nyingi za kesi ambazo mwisho wa siku kesi hizo wanashindwa
kutokana kuushindwa kuwa na uchunguzi wenye ushahidi.
Aidha
amesema kuwa baadhi ya mahakimu watakosa kazi kutokana na baadhi ya
kesi wameendesha kwa kupindisha na kuwapa washitakiwa haki wasio kuwa
nayo.
Waziri
Angela amesemaTakukuru wafanye kazi kwa waadilifu kwa kuwalinda watoa
taarifa ili waendelee kutoa taarifa kwa watu wanaojua kuwa wanahujumu
nchi kwa kutumia madaraka yao.
Amesema
watumishi wa Takukuru wana masilahi mazuri kuliko wa wafanye kazi
wengine ikiwa ni kuwaondoa katika ushawishi wa kuwa na tama kutokana
unyeti wa chombo hicho.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishina (CP), Valentino Mlowola amesema
wameokoa sh. Bilioni Saba (7) ambazo zilikuwa ziingie kwenye mifuko ya
wabadhirifu wachache ambao wanatumia nafasi zao vibaya kwa masilahi yao.
Amesema
walipokea malalamiko 4,675, uchunguzi uliokamilika wa majalada hayo ni
667, majalada yaliyokwenda kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP),
ni 278, majarada yaliyorejeshwa na DPP, ni 172 kwa ajili ya vibali
vya kufungua mashitaka na kesi mpya 314 nchini kote, na kesi
zilizoshinda 132 ambao wamefungwa na wengine kulipa faini.
No comments:
Post a Comment