MPANGO WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI WANUFAISHA KAYA MILIONI 1.1 NCHINI
Mpango
wa Kijamii wa Uzalishaji Salama ili kusaidia kaya masikini kupambana na
umasikini (PSSN) umefanikiwa kuwa na matokeo mazuri kwa kusaidia kaya
Milioni 1.1 nchini na kusaidia juhudi za serikali kupambana na
umasikini.
Hayo
yamefahamika wakati washirika wa maendeleo ambao ni Umoja wa Mataifa,
Benki Kuu ya Dunia, Serikali ya Uingereza kupitia kitengo cha Maendeleo
ya Kimataifa, Irish Aid, USAID, Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la
Sweden (SIDA) walipotembelea miradi ya maendeleo katika wilaya za
Unguja, Chamwino, Babati, Sumbawanga (Manispaa na Wilaya), Singida na
Hanang kwa kipindi cha siku tatu kuanzia Januari, 19 hadi 22.
Bi.
Kazijya Kila ambaye ni mmoja wa wanufaikaji wa fedha akitoa ushuhuda
kuhusu mradi wake wa chakula ulivyowezeshwa na TASAF ambapo hadi hivi
sasa anatengeneza faida ya Shilingi 7000 kwa siku na kabla ya kuwezeshwa
alikuwa akikaa nyumbani na mama yake bila kuingiza kipato chochote.
Katika
Mpango huo ambao utekelezwaji wake unasimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii (TASAF) unafanyika Tanzania Bara na Tanzania visiwani ukiwa na
lengo la kuzisaidia kaya masikini pesa za matumizi ili kukidhi mahitaji
ya kupata chakula pamoja na kuwawezesha kusaidia watoto wao kupata elimu
jambo ambalo linaonekana kuzaa matunda kwa maeneo mengi ikiwepo
Tanzania visiwani.
Serikali
ya Tanzania imekuwa ikisaidia na washirika wa maendeleo ili kupunguza
umaskini uliokithiri kwa wananchi wake na mwaka 2013 iliweka mpango wa
kusaidia kaya masikini 275,000 kwa kipindi cha miaka mitano na tangu
ianzishe mpango huo ilifanikiwa kusaidia kaya 275,000 kwa mwaka 2013
pekee katika wilaya nane nchini.
Mtaalamu
Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis
Abdulahi Mohamed (kushoto) na Msimamizi wa mpango wa PSSN, Bw. Ramadhani
Madari wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu kwa wanufaikaji wa
fedha hizo.
Na
mpaka kufikia sasa mpango huo umeshatoa malipo mara 12 na jumla ya kaya
masikini milioni 1.1 zimeshafaidika na mpango huo ikiwa ni kwa wilaya
161 na vijiji 9789 nchini.
Malengo
ya serikali ya Tanzania na mashirika ya kimataifa ni kuhakikisha
kufikia mwaka 2030 kunakuwa hakuna masikini hivyo ni wajibu wa kila nchi
kuhakikisha inawasaidia wananchi wake ili wajijengee uwezo wa
kujitegemea na kuondoka katika janga la umasikini.
Mkurugenzi
wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus
Kamagenge akizungumza na wanufaikaji wa mpango wa TASAF (hawapo
pichani).
Mkurugenzi
wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus
Kamagenge (kushoto) akifurahi jambo na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya
Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed.
Timu ya TASAF na wadau wa maendeleo wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment