MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YAZUKA TENA WILAYANI MVOMERO,MBUZI ZAIDI YA 70 ZAKATWA KATWA MAPANGA
Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa
jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati ya drafti),ikiwemo na
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro sambamba
na wananchi wakishuhudia tukio la mgogoro wa Wakulima na
Wafugaji,ambapo takribani mbuzi zaidi ya 70 wamekatwa katwa mapanga na
watu wasiojulikana,ambapo Waziri huyo ameahidi sheria na hatua za kudumu
za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba ametembelea Kijiji cha Kigurukwa mjini Morogoro kulikotokea mapigano ya Wakulima na Wafugaji yaliyosababisha kuuawa kwa mbuzi na Kondoo zaidi ya 70.Waziri Mwigulu ameagiza Kamati ya Ulinzi ya Mkoa kuhakikisha wote waliohusika katikla tukio hilo wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Pia ameagiza kutekelezwa haraka hukumu ya mahakama iliyotolewa mwaka 2005 iliyoagiza kuwekwa kwa mipaka kati ya eneo la wafugaji na wakulima.

Baadhi ya Mbuzi waliokatwa katwa na mapanga .
Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba akiongozwa na wafugaji
kabila la Wamasai kufuatia mgogoro wao na Wakulima na kupelekea
uharibifu mkubwa wa kuuwawa kwa wanyama zikiwemo mbuzi zaidi ya 70.
Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa
jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati la drafti),wakiwemo na
Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mvomero na wananchi mbalimbali
wakishuhudia tukio la kuuwawa kwa mbuzi zaidi ya 70 wakiwa wamekatwa
katwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Waziri huyo ameahidi sheria
na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero katika kijiji cha Kigurukwa mkoani Morogoro kufuatia mgogoro mkubwa kuzuka kati ya Wakulima na wafugaji,ambapo inaelezwa kuwa katika tukio
hilo mbuzi na kandoo zaidi ya 70 wakiwa wamekatwa katwa mapanga na
watu wasiojulikana.Waziri Mwigulu Nchema ameahidi kuwa sheria na hatua
za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment