KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA WARSHA YA KUHAMASISHA SHERIA MPYA YA UDHIBITI UZAGAAJI WA SILAHA NA RISASI NCHINI
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wa Warsha ya
Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa
Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Wapili
kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba.
Kulia ni Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za
Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti
Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa. Katika hotuba yake,
Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali
kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata
haijaanza. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi
wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba
akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria
Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa
wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam, kabla ya kumkaribisha Katibu
Mkuu ili aweze kuifungua warsha hiyo ya siku mbili. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwakilishi
wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na
Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa
Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa akizungumza na wajumbe (hawapo
pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na
Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar
es Salaam. Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa
Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba. Katibu Mkuu katika
hotuba yake ya ufunguzi wa warsha hiyo, aliwataka watu wanaomiliki
silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya
operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (wapili kulia) akitoka katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa
Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua Warsha ya
Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba, wapili
kushoto ni Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi-Makao Makuu, Hezron Gyimbi
na kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Yusuph
Ilembo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira akizungumza na wajumbe wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya
Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa
Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Katibu Mkuu
aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha
haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu
ya wajumbe wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha
na Risasi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani) wakati alipokuwa
akizungumza na wajumbe hao katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi
Oysterbay, jijini Dar es Salaam kabla ya kuwafungulia warsha yao ya siku
mbili itakayojadili umasishaji wa Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha ya
Mwaka 2015. Hata hivyo, katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu
wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka
iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (katikati waliokaa), Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara
hiyo, Marlin Komba (wapili kushoto waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi la
Polisi-Makao Makuu, Hezron Gyimbi (wapili kulia), Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP), Yusuph Ilembo (kulia) na kushoto ni
Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa
Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti
Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa, wakiwa katika picha ya
pamoja na washiriki wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa
Silaha na Risasi. Warsha hiyo ya siku mbili ilifunguliwa na Katibu Mkuu,
Rwegasira katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini
Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment