MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA CCM YAPAMBA MOTO MKOANI SINGIDA
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa maabara
katika shule ya Sekondari ya Unyianga,kata ya Unyianga mkoani
Singida.Shule hiyo mpya yenye madarasa manne ikiendelea kujengwa kwa
nguvu za wanannchi.
Sehemu ya jengo la ujenzi wa maabara ukiendelea kwa nguvu za Wananchi
Badhi
ya Wananchi waliokuwa wakishiriki ujenzi wa maabara hiyo,wakielekea
kumsikiliza Katibu MKuu wa chama cha CCM Ndugu Kinana aliyefika katika
shule hiyo ya sekondari ya Unyianga kushiriki ujenzi na kuwahimiza
wananchi kushiriki kujenga maendeleo yao.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa akiongozwa na mwenye shamba la Mtama
Bwa.Elisha Abdallah sambamba na Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mussa
Ramadhani alipokwenda kushiriki palizi la mkulima huyo wa mfano katika
kata ya Mtamaa,mkoani Singida
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pichani kati akisukuma jembe la Plau
linalokokotwa na N'gombe (kama aonekanavyo pichani) ikiwa sehemu ya
kushiriki palizi katika shamba hilo la Mtama lenye ukubwa wa Ekari moja
na nusu lililopo katika kata ya Mtama mkoani humo.Ndugu Kinana na
ujumbe wake yuko mkoani Singida kwenye maandalizi ya sherehe za
kuadhimishwa miaka 39 ya CCM,zinazotarajiwa kufanyika Februari 6 katika
uwanja wa Namfua mkoani humo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akitoa ufafanuzi kwa Wajasiria Mali hao mara
baada ya kusikiliza kero na malalamiko mbalimbali ambayo yanatakiwa
kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo,ili kuendana kasi ya Rais Dkt Joseph
Magufuli ya kuwahimiza wananchi kufanya kazi kwa kujituma kupitia kauli
yake ya Hapa kazi Tu.
Katibu
Mku wa CCM Ndugu Kinana akiwa katika ukumbi wa ofisi za chama mkoa
akisikiliza kero na mambo mbalimbali ya Wananchi ikiwemo kuyafanyia
kazi,Ndugu Kinana amekutana na wajasiriamali (Mama Lishe,Boda boda,Wauza
Mitumba na Wafanyabiashara nyingine ndogo ndogo.
No comments:
Post a Comment