ETHAD YAFUNGUA SEHEMU YA MAPUMZIKO KATIKA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA CHA ABU DHABI.
Mnamo
Mei mwaka huu, shirika la ndege la la Etihad linategemea kufungua sehemu
mpya ya mapumziko katika stesheni ya tatu ya uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Abu Dhabi kwa ajili ya wageni wake wa “Daraja la Kwanza”,
wasafiri wenye kadi maalum za Platinum za Etihad, wasafiri wenye kadi
maalum za Platinum kutoka washirika wa Etihad na wale watakaotumia
huduma ya “Makazi” iliyopo katika ndege zake aina ya Airbus A380. Etihad
imewekeza sana katika kutimiza lengo hili kwa ajili ya wageni wake wa
hadhi ya juu wanaopenda huduma zenye viwango bora zaidi.
Peter
Baumgartner, Afisa Mkuu wa Biashara, alisema: “Huduma hii itakuwa kito
katika taji letu hapa Abu Dhabi, ni nafasi nzuri kuonesha umahiri wetu
kwenye ubunifu na uvumbuzi. Ni muhimu kwetu kuhakikisha msafiri anapata
huduma bora kwanzia uwanjani hadi angani mpaka anaposhuka. Tuna imani
huduma na bidhaa tutakazotoa nje ya ndege zitajizolea umaarufu kama za
ndani ya ndege na tunategemea wateja watafurahia yote tunayowaandalia.”
Sehemu hii ya mapumziko itapambwa kwa mtindo wa Kiarabu na itaendana na umaridadi na umahiri uliozoeleka na kuhusishwa na jina la Etihad. Sehemu hii itaonesha uzoefu na ustadi wa Etihad na jinsi walivyojikita katika kuleta huduma yenye ukamilifu, kuanzia angani hadi ardhini
No comments:
Post a Comment