Waziri Muhongo :Ahadi ya Jan 15 Iko pale pale
Asteria Muhozya na Rhoda James, Mbeya
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesisitiza kauli yake kwamba tarehe iliyopangwa kati yake na Mameneja wa Tanesco nchi nzima ya kuhakikisha
inawaunganishinia umeme wateja waliolipa kwa kipindi kirefu ikiwemo
kukamilisha matatizo ya LUKU bado iko palepale.
“Katika hili nasema
kweli hakuna mzaha. Hatutanii. Wananchi wamechoka, wanataka umeme.
Mtindo wa kuandikiana barua tena haupo. Ukishindwa , unajiondoa
mwenyewe”,amesisitiza Prof. Muhongo.
Akijibu hoja za Kandoro
kuhusu suala la Makaa ya mawe, amesema atahakikisha suala hilo linapata
ufumbuzi wa haraka kuhakikisha rasilimali hiyo inatumika kama chanzo
kingine cha kuzalisha umeme nchini.
“Mkuu wa Mkoa hili
lazima tulishughulikie. Hatuwezi kuacha makaa ya mawe yakae tu kama
mapambo wakati tunahitaji sana nishati ya umeme kwa ajili ya kuondoa
matatizo ya umeme tuliyonayo”.
Prof. Muhongo ameongeza
kuwa, tayari amewaagiza wawekezaji wote wa makaa ya mawe wenye leseni
kukutana nae katika ziara ili kukubaliana kuhusu suala hilo.” Tayari
nimewaambia wote tukutane huku huku site wanieleze wanafanya nini”,
ameongeza
No comments:
Post a Comment