VIFUNGU VYA SHERIA YA NDOA VINAVYORUHUSU MTOTO WA KIKE KUOLEWA CHINI YA MIAKA 18 VYAPINGWA MAHAKAMANI.
Mwanaharakati
wa Haki za Binadamu, Rebeca Gyumi akizungumza jambo na Wakili
wakujitegemea, Jebra Kambole baada ya kutoka Mahakama Kuu ambako
wamefungua hauri la Kikatiba la kupinga sheria ya ndoa kifungu cha 13 na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kufunga ndoa.
Mwanaharakati
wa Haki za Binadamu, Rebeca Gyumi akizungumza na Waandishi wa Habari
nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kutoka Mahakamani hapo ambapo
wamefungua shauri la Kikatiba la kupinga sheria ya ndoa kifungu cha 13
na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kufunga ndoa, ambapo
wameona hiyo ni kumnyima mtoto wa kike haki yake ya msingi katika
jamii.
Wakili
wakujitegemea, Jebra Kambole kizungumza na Waandishi wa Habari nje ya
Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kutoka Mahakamani hapo ambapo
wamefungua shauri la Kikatiba la kupinga sheria ya ndoa kifungu cha 13
na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kufunga ndoa, ambapo
wameona hiyo ni kumnyima mtoto wa kike haki yake ya msingi katika
jamii.
Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
VIFUNGU
vya sheria ya ndoa vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka
18 vyapingwa mahakama kuu leo jijini Dar es Salaam.
Vipengele
vinavyopingwa ni kifungu cha sheria cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa
(CAP 29 R.E 2002), sheria inayotoa mwanya kwa mtoto wa kike kuolewa
akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakana na miaka 15 kwa ridhaa ya
wazazi ambayo ni kinyume na ibara ya 13, 12 na 18 ya katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania 19977 zinazotoa haki ya usawa mbele ya sheria
kutokubaguliwa, kuheshimu utu wa mtu na uhuru wa kujieleza.
Kesi
ya kupinga vifungu vya sheria ya ndoa vinavyoruhusu mtoto wa kike
kuolewa chini ya miaka 18 ni keshi ya kikatiba yenye namba tano ya
mwaka 2016 iliyofunguliwa na Mwanaharakati wa haki za binadamu, Rebeca
Gyumi na kusimamiwa na wakili Jebra Kambole wa Law Guards Advocate.
Akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam leo Mwanaharakati
wa Haki za Binadamu, Rebeca Gyumi ameomba mahakama kuu kufutia mbali
vifungu vya sheria hivyo na kupandisha umri wa chini wa kuoa kwa
wanaume na kuolewa kwa wanawake kuwa ni miaka 18.
Aidha Rebeca
amesema kuwa ndoa za utotoni kwa wasichana ni ukiukwaji wa haki za
binadamu pia kuzaa kwa msichana akiwa na umri mdogo ni chanzo kikubwa
cha matatizo ya Fistula na vifo vingi vya wajawazito.
No comments:
Post a Comment