POLISI MKOANI MWANZA YAKANUSHA KUHUSIKA NA UHALIFU
JESHI la Polisi mkoani Mwanza imekanusha kuhusika na uhalifu kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.
Hayo
yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) Justus Kamugisha alipokuwa akizungumza
ofisini kwake kuhusu tuhuma zilizotolewa juu ya Jeshi la Polisi mkoani
humo kuhusika na Uhalifu.
Kamanda
Justus Kamugisha amesema kuwa kuna taarifa zimekuwa zikitolewa na
baadhi ya vyombo vya habari kuwa Jeshi la polisi mkoani humo
linajihusisha na masuala ya uhalifu ikiwemo baadhi ya maofisa wao
kushirikiana na wahalifu katika uuzaji wa dawa za kulevya pamoja na
kushirikiana na majambazi kupora mali za wananchi .
“Ni
habari za uongo na za kulichafua Jeshi la Polisi na mimi kama Kamanda wa
Polisi nimelipokea suala hili kwa masikitiko na natoa onyo kwa vyombo
vya habari na jamii kwa ujumla kuacha tabia ya kueneza habari sizizokuwa
za kweli” Amesema Kamanda Kamugisha.
Aidha
Kamanda Kamugisha amesema kuna malalamiko yanayotolewa kuhusu Jeshi la
Polisi mkoani hapo kujihusisha na ulanguzi wa bidhaa zinazouzwa kwenye
kanteeni za Polisi, taarifa hizo ni za uongo kwani Serikali imeshafuta
msamaha wa kodi katika bidhaa hizo ambazo zilikuwa na bei tofauti na
zile zilizopo katika maduka ya kiraia.
Jeshi
la Polisi ni chombo cha ulinzi na usalama wa raia na mali zake hivyo
wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kupamabana
na uhalifu uliopo.

No comments:
Post a Comment