PINDA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UTAMADUNI WA WACHINA.
Mwambata
wa Utamaduni katika Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China Bw. Gao Wei akiongea na
waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano kuelezea maadhimisho ya sherehe
za mwaka mpya wa Kichina zitazofanyika Januari 30 mwaka huu jijini Dar es
salaam.
Waandishi
wa habari na wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa
Mwambata wa Utamaduni katika Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. Gao Wei
hayupo pichani wakati wa mkutano kuelezea maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya
wa Kichina zitazofanyika Januari 30 mwaka huu jijini Dar es salaam.PICHA
ZOTE NA ALLY DAUD -MAELEZO.
PINDA
MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UTAMADUNI WA WACHINA.
Na
Joseph Ishengoma
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Jumamosi ijayo
(30.01.2016) anatarajia kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kusherehekea mwaka
mpya wa Kichina.
Mwambata wa utamaduni katika ubalozi wa Jamhuri ya
Watu wa China nchini Bwana Gao Wei amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati
akiongea na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya utamaduni wa Wachina
nchini.
Maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina ni alama muhimu
katika utamaduni wa wachina na uadhimishwa kwa wachina kuungana pamoja na
familia zao na kufanya shughuli za kitamaduni ikiwemo michezo.
Bwana Gao Wei amaseme kuwa, maadhimisho ya mwaka
huu pamoja na kuwakutanisha jamii ya watu wa China na viongozi mbalimbali wa
serikali, yatatoa fursa za kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika,
kuendeleza urafiki uliopo na kuhakikisha kila upande unanufaika na urafiki huo.
“Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China pamoja na
watu wake tutaendelea kujenga mazingira rafiki kuhakikisha kila upande
unafaidika na urafiki wetu,” amesema.
Bwana Gao Wei ameongeza kuwa moja ya malengo ya
maadhimisho hayo hapa nchini ni kutoa ujumbe kuwa jamii ya Watu wenye asili ya
China wanakuwa watiifu kwa serikali ya Tanzania na kuleta usawa katika ushirikiano
wa kisiasa na biashara.”
Kwa mujibu wa Mwambata huyo, katika maadhimisho
hayo yatakayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja, Dar es Salaam, kutakuwepo na michezo mbalimbali ya utamaduni zikiwemo
nyimbo, muziki, judo, muziki wa ala, na michezo mingine ya kitamaduni.
Aidha Bwana Gao Wei ameeleza kuwa mbali na
maadhimisho hayo kufanyika Mnazi mmoja, pia yanatarajiwa kuadhimishwa katika
miji mingine ya Arusha, Dodoma na Mwanza katika siku tofauti tofauti.China ilianza kuadhimisha sherehe hizo tangu karne
ya 12 ambapo kwa mwaka huu, kilele cha sherehe hizo ni February 8, 2016.
No comments:
Post a Comment