MWAKA MWINGINE WA MAENDELEO MAKUBWA KWA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD.
SHIRIKA
la ndege la taifa la umoja wa falme za nchi za kiarabu la Etihad
limefurahishwa na ufanisi na utendaji wa operesheni zake kwa mwaka wa
2015 zilizowafanikisha kufikia malengo yao ya ukuaji ambapo sasa
wanabeba abiria wengi na mizigo mingi zaidi ya awali.
Mwaka
jana Shirika lilibeba abiria milioni 17.4, sawa na asilimia 17 zaidi ya
mwaka 2014, wakiendesha safari 97,400 za ndege zilizofikisha jumla ya
kilomita milioni 467.
Hii
ni dhahiri kwamba abiria walifurahia huduma hizi na hivyo uhitaji
uliongezeka, jambo ambalo lilisisitiza nguvu ya mikakati ya ukuaji
iliyowekwa na shirika la ndege la Etihad.
Kwa
ujumla, ndege za Etihad pekee zimebeba zaidi ya asilimia 75 ya abiria
waliosafiri kwenda na kuondokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu
Dhabi katika mwaka wa 2015. Etihad pamoja na washirika wake walio na
ndege zinazofika mji huo mkuu wa UAE wamefikisha jumla ya asilimia 84 ya
abiria waliotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi.
Yote haya yametokana na huduma zetu zinazokidhi viwango vya kimataifa ambazo pia zimejizolea tuzo mbalimbali. Pamoja na hayo, mashirika mengi yanavutiwa kujiunga nasi na tunazidi kuongeza idadi ya washirika wetu, kukuza ukubwa wa mitandao yetu ili kufika sehemu nyingi zaidi duniani.
No comments:
Post a Comment