Header Ads

Benki ya Exim yaibuka na ushindi katika mechi ya ligi ya mabenki


Kikosi cha timu ya soka ya Benki ya Exim Tanzania ambacho kiliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Benki ya Akiba katika mechi ya pili ya ligi ya mabenki iliyofanyika katika Viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Klabu ya soka ya Benki ya Exim imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Benki ya Akiba katika mechi ya pili ya ligi ya mabenki iliyofanyika katika Viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Wafanyakazi wa benki hizo na mamia ya mashabiki wa mpira walijitokeza uwanjani hapo kuzishangilia timu hizo katika mechi yenye ushindani ushindani mkali iliyoshuhudia dakika 90 zikimalizika huku Timu ya Benki ya Exim ikiibuka vinara katika mtanange huo.

Ligi hiyo, inayoshirikisha benki zaidi ya 16, inalenga kuimarisha urafiki na ushirikiano baina ya mabenki licha ya kuwa washindani kibiashara.

“Benki ya Exim iliona umuhimu wa kushiriki katika ligi hii kwani ni nafasi ya kipekee sana kutambua umuhimu wa jamii ya benki katika kuleta maendeleo kwenye taifa letu. Lakini pia michezo ni afya, na kwa kushiriki katika ligi hii tunawapa fursa wafanyakazi wetu kuimarisha afya zao kupitia mazoezi,” alisema Bw Greyson Malisa, Meneja Msaidizi rasilimali watu wa benki ya Exim.

Ligi ya mabenki ilizinduliwa mwishoni mwa mwezi Novemba 2015 na inatarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa mwezi huu ambapo washindi wataibuka na zawadi mbalimbali zikiwemo medali.

“Shukrani za dhati ziwaendee wachezaji waliotoa muda wao na kuweka juhudi, ujuzi na nguvu zao ili kupata ushindi huu. Nawasihi wachezaji waendeleze juhudi hizi ili tuweze kuibuka washindi wa jumla katika mashindano haya,” alihitimisha.

No comments:

Powered by Blogger.