Mbwana Samatta akutana na Mufti Mkuu Sheikh Zuberi
Mwanasoka
Bora Afrika Ndg. Mbwana Samatta akikabidhiwa baadhi ya zawadi
mbalimbali na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi
kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.
Leo
tarehe 11 January 2016, Mwanasoka Bora Afrika Ndg. Mbwana Samatta
alimtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi
kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.
Mufti
Mkuu mbali na kumpatia zawadi mbalimbali kwa ajili ya kumsaidia katika
imani yake pia alipata nafasi ya kumuombea dua ya mafanikio zaidi huko
aendako Ulaya na kumpa nasaha asisahau kumuomba Mwenyezi Mungu kila
wakati na kufanya ibada muda wote atakaokuwa nje ya mazoezi.
Mwisho Mufti alimtakia mafanikio mema na kumuambia dua za watanzania wote zipo naye.
No comments:
Post a Comment