MBUNGE WA JIMBO LA NYAMAGANA KUKOMALIA UJENZI WA MAEGESHO JJINI MWANZA.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula.
Na:George Binagi.
MBUNGE
wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus Mabula (CCM, ameahidi
kushughulikia suala la ujenzi wa maegesho ya magari makubwa ya mizigo
nje ya jiji la Mwanza ili kuzuia magari hayo kuingia katikati ya jiji.
Akizungumza
ofisini kwake hii leo, Mabula amebainisha kuwa upo mpango wa kujenga
maegesho hayo katika maeneo yaliyo nje ya Jiji la Mwanza, hatua ambayo
itasaidia magari hayo kutoingia katikati ya Jiji na hivyo kuondoa
malalamiko yaliyopo kutoka kwa madereva wa magari madogo ya mizigo
wanaolalamikia uingiaji wa magari makubwa ya mizigo katikati ya jiji.
Ameyataja
maeneo yanayotarajiwa kujengwa maegesho hao kuwa ni Buhongwa pamoja na
Igoma na kwamba baada ya ujenzi wake kukamilika, magari yote makubwa ya
mizigo hayataruhusiwa kuingia katikati ya Jiji.
Mabula
ambae alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza katika uongozi
uliomalizika mwaka jana, amebainisha kuwa utekelezaji wa ujenzi wa
maegesho hayo unatarajiwa kufanyika kwa uharaka zaidi ambapo amewahimiza
wawekezaji mbalimbali kujitokeza ili kushirikiana na halmashauri ya
Jiji la Mwanza kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo.
Suala
la magari makubwa kuingia katikati ya Jiji la Mwanza huku yakiwa na
mizigo, linalalamikiwa na madereva wa magari madogo ya mizigo kwa kile
wanachoeleza kuwa wanaingiliwa katika shughuli ambazo wao wangezifanya
na hivyo kujiingia kipato ambapo wameiomba halmashauri ya Jiji la Mwanza
kutoruhusu magari hayo kuingia katikati ya Jiji.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari ofisini kwake
No comments:
Post a Comment