KAMPENI YA UWEKAJI AKIBA FNB YAFIKIA TAMATI.
Mkuu
wa Masoko wa First National Bank, Blandina Mwachanga (kulia) akiongea na
waandishi wa habari baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni tano
kwa Peter Kimune (katikati) mshindi wa kampeni ya uhamasishaji kuweka
akiba iliyokuwa ikiendeshwa na benki hiyo kwa muda wa miezi mitatu.
Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za reja reja wa benki hiyo
Francois Botha.
(Picha Mpiga Picha Yetu)
KAMPENI
ya kuhamasisha Watanzania kujiwekea akiba zaidi iliyokuwa ikiendeshwa
na First National Bank Tanzania kwa miezi miatu imefika mwisho huku
mshindi wa tatu na wa mwisho akikabidhiwa zawadi ya shilingi milioni
tano.
Akizungumza
kwenye hafla ya kuhitimisha kampeni hiyo na kumkabidhi zawadi Peter
Kimune, mkazi wa Dar es salaam aliyeibuka mshindi wa mwezi Disemba 2015,
Mkuu wa kitengo cha rejareja cha benki hiyo, Francois Botha alisema
“imekuwa kampeni ya yenye mafanikio makubwa na ni furaha kuona wateja
wengi wakijitokeza kushiriki.” “Kampeni hii haikuwa tu shindano bali pia
imetoa somo na kuhamasisha Watanzania wengi kujitokeza kwenye kuweka
akiba. FNB inaamini kwamba kupitia kampeni hii imeweza kuhamasisha
Watanzania kuweka akiba kwa ajili ya mustakabali salama wa kifedha hapo
badae.
Akiba
inaleta uwezo wa kuwekeza siku zijazo na husaidia wakati wa dharula au
pale unapotaka kutimiza mipango yako,” alisema Botha. Kampeni hiyo ya
uwekaji akiba ilizinduliwa Oktoba, 2015 na kwa miezi mitatu imeweza
kutoa nafasi kwa wateja wapya na wa zamani kuingia moja kwa moja kwenye
droo kutokana na kila shilingi elfu hamsini waliyoweka kwenye akaunti
zao.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni tano, mshindi huyo
aliishukuru benki hiyo kwa kuanzisha mpango huo na kuongeza kuwa uwekaji
akiba ni muhimu katika uhifadhi wa fedha binafsi na pia husaidia katika
kujenga jamii imara yenye uhakika wa kuishi maisha bora.
No comments:
Post a Comment