WAZAZI/WALEZI WAASWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akizungumza na waandishi wa habari Katika ukumbi wa Maendeleo ya Jamii,
Jisia, wazee na watoto jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuhamasisha
wazazi au walezi kuwahamasisha waoto kujiunga na shule za Msingi na
Sekondari kwa 2016.
kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa na Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
SERIKALI
itawafungilia mashtaka na kuwapeleka mahakamani wazazi na walezi wote
watakashindwa kutimiza wajibu wao wa kuwapeleka watoto shule ili kupata
Elimu ya Msingi na Sekondari.
Pia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ikishirikiana
na Ofisi ya Rais- TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi, Technologia, na
Ufundi inawahamasisha wazazi au walezi kutimiza wajibu wao kuhakikisha
kuwa watoto wenye umri wa kuanza shule za msingi na Sekondari kuanza kwa
wakati.
Hayo yamesemwa na Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Pia viongozi na watendaji wa mikoa na halmashauri, maafisa Maendeleo ya jamii na watendaji wa kata wameaswa kusimamia na kutekeleza
majukumu yao kwa kuhakikisha wanahamasisha jamii ipasavyo juu ya watoto
kujiunga na darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa mwaka huu.
Ummy
amesema kuwa maafisa wa maendeleo ya jamii za mikoa, Halmashauri na kata
zote hapa nchini watoe taarifa za utekelezaji wa jambo la watoto
kwenda shule mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.
Aidha
Serikali inatoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wote
wanaendelea na masomo ya shule ya Msingi na Sekondari vizuri na
wahudhurie masomo yao kwa ufanisi, pia serikali haitegemei kuona utoro
wa watoto mashuleni kutokana na sababu zinazoweza kuepukika.
No comments:
Post a Comment