Cannavaro kukabidhi barua ya kujiuzulu Stars leo
Nahodha na beki wa zamani wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Wilbert Molandi
Dar es Salaam
MUDA mfupi baada ya kutangaza kustaafu kuichezea Taifa Stars, nahodha na beki wa zamani wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ leo Jumamosi anatarajia kukabidhi barua rasmi ya uamuzi wake huo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Hiyo
ni siku moja tangu atangaze kujiuzulu kuichezea timu hiyo baada ya
Kocha Boniface Mkwasa kumpokonya unahodha na kumabidhi Mbwana Samatta.
Samatta alitangazwa kuwa nahodha na Mkwasa mara baada ya kushinda uchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka Afrika.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Cannavaro alisema, atakabidhi barua hiyo baada ya kukutana na washauri wake na kuandika barua hiyo na leo asubuhi kuipeleka TFF.
Cannavaro alisema; “Nimepokea maoni mengi kutoka kwa wadau wa soka na wote wanataka nibadili uamuzi ili niendelee kuichezea Stars.
“Kwanza niseme nimechoka kuichezea Stars, muda niliouchezea unatosha kabisa kwangu, hivyo ni wakati wa kuwaachia wengine waendelee kuichezea timu kwa mafanikio.
“Sitabadili uamuzi na kesho (leo) asubuhi nitafika kwenye ofisi za TFF kwa ajili ya kukabidhi barua kuwataarifu rasmi kwamba mimi nimejitoa Stars ili nitoe nafasi kwa wengine,” alisema Cannavaro kwa masikitiko makubwa.

No comments:
Post a Comment