NSSF YASHIRIKI MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA ABITAT JIJINI DAR ES SALAAM
Ofisa
Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mselem
Mwanamsoga akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka
Wizara ya Viwanda na Biashara, Edward Sungura (kulia), wakati wa
Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyoandaliwa na Umoja wa
Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki (Abitat), yanayoendelea katika
Ukumbi wa Diamond Jubilee. (Picha na Francis Dande).
Ofisa
Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Aisha Sango (wa pili kulia), na Ofisa Uwekezaji wa NSSF, Mselem Mwanamsoga wakitoa maelezo kuhusu huduma wanazotoa, ikiwemo uuzwaji wa viwanja vilivyopimwa katika eneo la Kiluvya, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, kwa
watu waliofika katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyoandaliwa
na Umoja wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki (Abitat),
yanayoendelea katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Baadhi ya watu wakipata huduma katika banda la NSSF.
No comments:
Post a Comment