MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO, KATIKA KITUO CHA KUTUNZIA KUMBUKUMBU CHA TAIFA (NATIONAL INTERNET DATA CENTRE) KIJITOMYAMA.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifunua kitambaa kuzindua Jengo jipya la Mradi wa Kituo cha Kutunzia
kumbukumbu Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, wakati wa
hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika leo Kijitonyama, jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame
Mbarawa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib,
akipata maelezo kuhusu utendaji kazi wa mitambo ya kutunzia kumbukumbu,
kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Bidhaa za Shirika la Simu
Tanzania, TTCL, Issaya Ernest, wakati Dkt Bilal, alipotembelea kituo
hicho cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Internet Data Centre)
Kijitonyama, leo Okt 21, 2015.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa, kwa
pamoja wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kutunzia
kumbukumbu cha Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, leo
Okt 21, 2015.
No comments:
Post a Comment