NAIBU WAZIRI WA MAJI, AMOS MAKALLA AITIMISHA ZIARA YAKE YA SIKU TATU KATIKA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO YA UJENZI WA MAJI MKOA WA DAR ES SALAAM
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia), akisalimiana na Afisa Ugavi Mkuu
wa Bohari Kuu ya Maji, Datus Bahati mara baada ya kuwasili Bohari Kuu ya
Maji wakati wa ziara yake ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa miradi
ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji
Safi na Maji Taka mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) ambapo aliitimisha
ziara hiyo Agosti 27, 2015 kwakukagua miradi iliyopo daraja la mpiji na
Kerege na maungio ya maji ya wazo.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya
Bohari Kuu ya maji iliyoko Boko jijini Dar es Salaam wakati ziara yake
ya siku ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar es
Salaam inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Dar es
Salaam (DAWASA).
Afisa
Ugavi Mkuu wa Bohari Kuu ya Maji, Datus Bahati akisoma taarifa ya
utekelezaji wa kazi za Bohari Kuu ya Maji kwa Naibu Waziri wa Maji, Amos
Makalla (hayupo pichani).
Kushoto
ni Meneja Usimamizi Uendeshaji na Mazingira DAWASA, Modesta Mushi,
Afisa Ugavi Mkuu wa Bohari Kuu ya Maji, Datus Bahati (kulia) pamoja na
Wakandarasi wa miradi hiyo na maofisa kutoka Wizara ya maji na waandishi
wa habari wakimskiliza Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla wakati
akizungumza (hayupo pichani).
No comments:
Post a Comment