Header Ads

TIMU YA WATU 39 KUTOKA AFRIKA KUSINI WAPNDA MLIMA KILIMANJARO KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA KUSAIDIA KUNUNUA TAULO MAALUMU KWA WASICHANA WALIOPO MASHULENI PINDI WAWAPO KATIKA HEDHI.

Timu ya watu 39 wakiwasili katika lango la Marangu tayari kuanza Changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia kununua taulo maalumu kwa wasichana waliopo shuleni zisaidie wakati wanapokuwa kwenye siku zao za Hedhi.
Katika timu hiyo wamo wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za nchini Afrika Kusini ,watu maarufu ,watangazaji katika vituo vya Luninga,wachezaji filamu n.k. katikati hapo ni Ofisa Uhusiano wa nje wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom nchini Afrika kusini,Maya Makanjee.
Muigizaji maarufu wa filamu,Jack Devnarain akijulikana kama Rajesh Kumar katika tamthiliya ya Isidindo the Need akiwasili katika lango la Marangu tayari kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi mkuu Hfadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Erastus Rufunguro akizungumza wakati akitoa historia fupi ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya washiriki katika changamoto hiyo.
Mwanzilishi wa taasisi ya Imbumba Foundation ,Richard Mabaso akizungumza lengo la safari hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro ijulikanao kama Trek4 Mandela ambayo ni mahususi kwa ajili ya kuchangisha fedha zausaidia wasichana walioko mashuleni.
Baadhi ya washiriki katika changamoto hiyo.
Katibu tawala wilaya ya Moshi ,Remida Ibrahim akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya katika hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya wageni hao kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.

No comments:

Powered by Blogger.