WAKUU WA TAASISI ZA TAKWIMU WA NCHI ZA AFRIKA WAKUTANA JIJINI DAR
Mtendaji
Mkuu wa Taasisi ya Takwimu ya Bara la Afrika Bw. Joseph ILboudo
akizungumza na watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu Kongamano la
Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala lililowahusisha wataalam na Wakuu wa
Taasisi za Takwimu wa nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya
Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam.
Bw. Andry Andriantseheno kutoka UNECA akiongoza kongamano hilo la siku 2 la watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu wa nchi za Afrika linalojadili masuala ya Uongozi na utawala na leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka Tanzania wenyeji wa mkutano huo.Baadhi ya watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala linaloendelea jijini Dar es salaam.Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Takwimu Barani Afrika (AFRISTAT) pia mtaalam wa Takwimu kutoka nchini Cameroon Bw. Martin BALEPA akiwasilisha mada kuhusu namna nchi za Bara la Afrika zinavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kutumia takwimu sahihi.
No comments:
Post a Comment