UNESCO YAFURAHIA MABADILIKO REDIO JAMII
Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akiendesha
mafunzo ya matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na kupokea habari
yaliyofanyika katika kituo cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza chini
ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa ushirikiano na
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph akitoa
maelekezo kwa vikundi kazi wakati mafunzo hayo.
Miongoni
mwa washiriki wa semina ya mwisho Pili Mlindwa wa redio jamii ya Panga
FM akizungumzia mafunzo waliyopewa katika matumizi ya Tehama, alisema
yamembadili sana katika utendaji wake na kumuongezea maarifa ya kazi. Alisema
amefurahishwa sana na mafunzo ya Tehama ambayo sasa anaweza akafanya
kazi nje ya studio na bado mhariri wake akawa na taarifa yake na
kuitumia.
Alisema
mafunzo mengi aliyopata katika mradi huo yakiwemo pia ya matumizi ya
meseji Matrix, simu za mkononi kukusanya na kutoa taarifa kumemfanya awe
wa kujiamini. Naye
mwandishi wa habari, Bakari Khalid wa redio jamii Kaham FM ya Shinyanga
akizungumzia Mafunzo ya Tehama alisema kwamba Unesco imefanya jambo la
maana kuwapa mafunzo hayo ikizingatiwa kwamba redio nyingi zina watu
wasiopitia chuo.
Alisema kwa sasa wanaweza kutengeneza vipindi bora vya kuhamasisha afya, elimu na kilimo na namna ya kuandika habari. Aidha alisema sasa wana uwezo wa kutumia kompyuta mpanguso (tablet) katika kuandaa vipindi na pia kuandaa taarifa mbalimbali.
Wakala
wa habari wa kituo cha Orkonerei Radio Service (ORS) cha wilayani
Simanjiro, Nyangusi Ole Sangida akichangia mada kuhusu changamoto
zinazowakabili Mawakala wa Redio Jamii katika ukusanyaji wa habari
wakati wa mafunzo ya matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na kupokea
habari yaliyofanyika katika kituo cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza
chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa
ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni
(UNESCO).
Wakala
wa habari wa kituo cha redio jamii Pangani FM, Pili Mlindwa akichangia
mada wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku nne ikiwa ni sehemu ya mradi
wa SIDA wa kuwajengea uwezo katika kuwawezesha kutengeneza vipindi bora.
Wakala
wa habari wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Paulina Juma
akiwasilisha kazi ya kikundi ya kuandaa habari na kurekodi kipindi
waliyofanya kwa vitendo katika Kompyuta mpanguso (Tablet) walizokuwa
wakitumia kwenye mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment