MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AMPONGEZA MWENYEZI MUNGU KWA KUSHUSHA MVUA ILIYOZAA MAFURIKO.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick
amezipongeza mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam,
kwa mvua hizo kuisaidia serikali katika utekelezaji wa hukumu ya
mahakama kuu, kuwaamuru wakazi wa mabondeni kuhama kwa lazima.
Wananchi waligoma katakata kuhama huku serikali ikijishauri namna ya kuwahamisha watu kwa nguvu bila kuleta madhara, haswa kwa kuzingatia mwaka huu ni wa uchaguzi.
Mvua hizo zinazoendelea kunyesha na zimeisaidia serikali kwa kiasi kikubwa kuwahamisha wananchi hao.
Mkuu huyo wa Mkoa, ametoa shukrani hizo, katika mahojiano ya moja kwa moja katika kipindi cha Kumepambazika, kinachorushwa na Redio One Stereo asubuhi leo.
Alisema kuwa imetokea taarifa za kupoteza maisha kwa watu wengine wawili, mmoja akisombwa na maji wakati alipotaka kuvuka mto Ng'ombe na kumzidi nguvu na kumsomba wakati mwingine ni mtoto mdogo wa miaka miwili aliyekuwa akicheza nje ya nyumba yao ambapo maji ya mafuriko hayo yakapita mbele ya nyumba na kumsomba.
Kuhusu wakazi wa mabondeni, Sadiki alisema kuwa baada ya mafuriko ya 2011, serikali iliwahamisha wananchi na kuwapatia viwanja Mbweni huku baadhi yao wakihama na wengine wakigoma na kwenda mahakamani ambapo serikali ililazimika kutowahamisha kwa nguvu.
Hoja za wakazi hao kupingwa kuhamishwa ni kwa sababu wametumia gharama kubwa katika ujenzi na kuwekewa huduma muhimu za maji na umeme, hivyo hawawezi kuhama bila kufidiwa.
Mahakama tayari imetoa maamuzi ya kuwataka wananchi kuhama huku serikali ikijipanga kutumia nguvu kuwahamisha tena bila kuwapatia maeneo mbadala.
Lakini kabla ya utekelezaji wa zoezi hilo, mkuu huyo alieleza kuwa Mwenyezi mungu amepeleka mvua iliyosaidia na kutoa msaada kwa serikali kuwahamisha wananchi na kuipunguzia serikali kazi ya kuwahamisha kwa nguvu.
Mkuu wa Mkoa alisema kuwa baada ya usaidizi huu wa mvua kwa kuwahamisha watu hao, sasa serikali imebakiwa kazi ndogo tuu ya kuhakikisha watu hao hawarudi tena katika maeneo hayo na kuwasisitiza wale wote waliohama na kubakiza baadhi ya vifaa vyao, mvua zikisimama wataruhusiwa kivichukua kabla ya kupitisha tingatinga na kulisawazisha eneo lote kubaki tambarare kama walivyofanya kwa eneo la Kipawa.
Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam ameviomba vyombo vya habari kutoa ushirikiano katika zoezi hili kuhakikisha wakazi wa mabondeni wanahama kwa ridhaa yao kutekeleza amri ya mahakama na wale wote watakao kaidi, watahamishwa kwa nguvu.http://www.jamiiforums.com

No comments:
Post a Comment